DAMPO LA TAKA LAENDELEA KUZIGOMBANISHA HALMASHAURI MBILI NJOMBE

Na Amiri kilagalila-Njombe

Baadhi ya madiwani akiwemo diwani wa kata ya Saja wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe Adrew Mangula wamelitaka baraza la madiwani la halmashauri hiyo kuridhia hoja ya kutaka Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania atoe tamko rasmi juu ya matumizi ya dampo lilipo katani kwake linalotumiwa na halmashauri ya mji wa Makambako licha ya malalamiko yao kufikishwa kwa naibu waziri wa mazingira na baraza la taifa la mazingira(NEMC).

Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani katika halmashauri hiyo,diwani huyo amesema kuwa anashindwa kuelewa kinacho endelea juu ya matumizi ya dampo hilo kwa kuwa naibu waziri wa mazingira na baraza la taifa la mazingira lilitoa zuio kwa halmashauri ya mji wa makambako kutotumia dampo hilo lakini bado linaendelea kutumika.

“Hivi ni waziri wa namna gani ambaye anaweza kuja kusema ,mimi naona sasa hivi anayeweza kusema neno ni Rais mwenyewe wa jamhuri ya muungano wa Tanzania,labda mwenyekiti uridhie  kwa baraza lako hili tukufu kwamba Rais aseme neno ili kuwaokoa wananchi wale wa Itengeru na Saja maana yake hata sielewi nani anaweza kusema ni mkuu wa wilaya,mkuu wa mkoa, ni waziri ama ni nani mimi naona amebaki Rais”alisema diwani Mangula

Aidha madiwani wa halmashauri hiyo wamesema hatua za haraka zinatakiwa kuchukuliwa ikiwemo kufika mahakamani na kwenda kufunga dampo hilo ili kuwanusuru wananchi wao na athali ambazo zinaweza kujitokeza hapo baadae hususani magonjwa ya mlipuko.

“Sisi tunaona kuna mtu anafumba macho kwa maslahi yake,eneo lile lipo ndani ya halmashauri yetu tunajitambua sisi ndio wenyewe tununue makufuri tukafunge tuandike bango litakaloonesha ni marufuku kutumia hili”walisema madiwani

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe Antony mawata amesema anashangazwa na kitendo cha halmashauri ya mji wa Makambako kuendelea kutumia dampo hilo licha ya zuio la naibu waziri na athali ambazo zinaweza kuwapata wananchi wa Saja.

“Ivi mamlaka yanayoendelea kutumia na kubeza nini na mkurugenzi wa Makambako nimewahi kumsikia akisema sasa tumeshapanga na tumeingiza kwenye bajeti na tunahela ya kwenda kutengeneza mifereji ili tuendelee kutumia hii sio sawa hawa wamepanga kutudhulumu na kuendelea kutuulia watu wetu”alisema Mawata

Hata hivyo hii leo hoja za madiwani wa halmashauri hiyo zimeibuka katika baraza la madiwani halmashauri ya mji w Makambako huku mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa makambako Hanana Mfikwa akisema kuwa wao wanaendelea kutumia dampo hilo kutokana na kibali halali ambacho wamekipata kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Njombe,na hakuna barua yoyote ambayo wameipata ya kuzuia wasiendelee kutumia dampo hilo.

“Kimsingi lile dampo ni la halmashauri yetu na lilijengwa na hao hao wanaolalamika wakiwa Wanging’ombe lakini wote tukiwa Njombe tulipanga kwa pamoja tukajenga hilo dampo,kwa hiyo sisi kama Makambako tulipewa barua rasmi na mkuu wa mkoa kwamba tutupe taka pale kwa hiyo tunategemea kupata barua kwa vyombo vyenye mamlaka,Nemc wamekuja ni sahihi lakini kama hawajatoa waraka wowote  kusimama kutupa taka pale sisi hatuwezi kusimama,lakini kimsingi lile dampo liko salama na wala halina madhara kwa kuwa hata wenyewe wanaweza kutumia”alisema  Hanana Mfikwa

Joseph Makinga ni katibu tawala msaidizi osifi ya Rais na serikali za mitaa tamisema mkoa wa Njombe,akizungumza katika baraza la madiwani halmashauri ya mji wa Makambako amesema kwa sasa swala hilo lipo mezani kwa mkuu wa mkoa wa Njombe lakini waendelee kuwa na subira kwani bado halijashughulikwa.

Zaidi ya miaka mitano sasa kumekuwa na mgogoro kati ya h almashauri hizo kuhusu matumizi ya dampo hilo


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post