BRELA KUTOA LESENI ZA BIASHARA DARAJA A KWA WASAFIRISHAJI WA MAZAO NA MIFUGO NJE YA NCHI KWENYE MAONYESHO YA NANE NANE

 Afisa kutoka kitengo cha Miliki Bunifu wa Brela Suzana Senzo kulia akimsikiliza kwa umakini mmoja wa wananchi aliyefika kwenye banda lao kwenye maonyesho ya wakulima nane nane yanayoendelea mkoani Simiyu
NAIBU Waziri wa Viwanda Mhandisi Stella Manyanya kulia akipata maelezo kutoka kwa maafisa wa wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (Brela) mara baada ya kutembelea banda lao



WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (Brela) wamesema kwamba wameamua kushiriki kwenye maonyesho ya kilimo ya nane nane yanayoendelea mkoani Simiyu kwa ajili ya kuwapasha habari wakulima na wafanyabiashara kupata huduma ya leseni hizi ili kuweza kutoa huduma hata katika masoko ya nje 

Hayo yalisemwa na Afisa kutoka kitengo cha Miliki Bunifu wa Brela Suzana Senzo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya wakulima nane nane yanayofanyika mkoani Simiyu. 

Alisema wameamua kushiriki kwenye maonyesho hayo hasa ukizingatia kauli mbiu ya mwaka huu ya nane nane ni Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa ukuaji wa uchumi wa nchi pamoja dhima ya kujenga uchumi wa viwanda. 

Suzana alisema hivyo vyote vinaenda sambamba na uwezeshaji biashara huku akieleza lengo kubwa la mfumo ni kuhakikisha wakulima na wazalishaji wa bidhaa nchi wanapata taarifa za mahitaji ya masoko ya nje . 

“Kwa mfano mtu anataka kusafirisha bidhaa kupeleka Ulaya ,ni rahisi sana kupata taarifa hizi katika mfumo wa trade facilitation information module ambapo hapo awali haikuwepo kabisa”Alisema 
Alieleza kwamba wanataka wakulima,wafanyabishara wapate taarifa moja kwa moja kutoka mkoani Simiyu katika viwanja vya nane nane.

Aidha alisema kwa mkoa huo wafugaji wengi hivyo wafugaji ni wengi hivyo ukitaka kujua taarifa zinazohusu vibali na leseni mbalimbali katika kupeleka mifugo yake katika soko la nje ni rahisi kwasababu taarifa zipo ambazo zitamuwezesha kujua nini anahitaji, kwa gharama gani, itachukua muda gani, aendee taasisi gani na iko wapi. 

Aliongeza kwamba kwa mantiki hiyo mfumo huu ni mwarobaini wa tatizo la taarifa za kibiashara katika upatikanaji wa vibali na leseni mbalimbali nchini huku wakiwakaribisha wananchi kufika kwenye banda lao kupata huduma hizo. 

“Lakini pia BRELA tunatoa leseni za kundi A kama zilivyoainishwa katika sheria Leseni za Biashara ya Mwaka 1972 na marekebisho yake…. Leseni za kundi A ni zipi, ni zile leseni zinazotolewa kwa biashara zenye mlengo wa kitaifa, kimataifa na zenye usimamizi maalum, biashara hizi ni kama usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi, uingizaji wa bidhaa ndani ya nchi na biashara za usimamizi maalum kama za madini, benki na zingine kama hizo. 

Awali akizungumza Afisa kutoka kitengo cha Miliki Bunifu wa Brela suzana Senso amesema wapo kwenye maonyesho hayo kwa ajili ya kuwapasha habari wakulima na wafanyabiashara kupata huduma ya leseni hizi ili kuweza kutoa huduma hata katika masoko ya nje (internatinal market) . 

Hivyo bas mkulima / mfanyabiashara akifika BRELA anapata taarifa za kibishara zaidi katika biashara za kimataifa,asajili kampuni au jina la biashara na anapata leseni itakayomuwezesha kusafirisha bidhaa zake nje ya nchi. 

Hata hivyo alisemwa kwamba kwa matiki hiyo sasa Brela ni one stop shop mfanyabiashara akifika hapa anapata kila kitu kitakachomuwezesha kwenda kufanya biashara duniani. 

Naye kwa upande wake Eliabu Rwabiyago ambaye ni Afisa kutoka Brela amesema wakala pia ina kitengo cha kuwezesha biashara (trade facilitation section) ambacho kimejikita katika uwezeshaji biashara. 

Alisema kwa sasa wakala huo unaandaa portal inayoitwa trade facilitation information module , portal ambayo itajikita katika kutoa taarifa za kibiashara nchini. 

Alisema kwasababu wafanyabiashara wengi nchini na nje ya nchi wanataka kufanyabiashara lakini taarifa za kibiashara kwa maana ya vibali na leseni mbalimbali zinazohitajika zinapatikanaje na kwa muda gani hivyo kwa mtandao hayo maswali yote yamejibiwa. 

Alieleza kwamba kukamilika na kutumika kwa mfumo huu kutakuwa na faida nyingi sana katika uwezeshaji wa biashara ikiwemo kuongeza uwazi katika utoaji wa huduma za umma, kuiongeza ushirikiano baina ya ofisi za umma na wafanyabiashara maana kwa kutumia mfumo watakuwa wanaweza kaundika maoni na maswali yao kujibiwa moja kwa moja, 

Alisisitiza pia kwamba pia mfumo huu unatumika kama promotional tool kwa maana bidhaa ambazo tunataka ziende duniani kirahisi zinawekwa katika mfumo na wafanyabiashara wanazipata kirahisi, kupunguza gharama za ufanyaji wa biashara na kuboresha mazingira ya biashara kwa ujumla. 

Mpaka sasa BRELA wameweza kuweka taarifa ya bidhaa 26 za kupeleka nje ya nchi (export) na 13 za kuingiza ndani ya nchi (import) 

Mwisho.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527