ALIYEDAIWA KUMUUA MKEWE KWA SHOKA APIGWA NA KUCHOMWA MOTO | MALUNDE 1 BLOG

Monday, August 26, 2019

ALIYEDAIWA KUMUUA MKEWE KWA SHOKA APIGWA NA KUCHOMWA MOTO

  Malunde       Monday, August 26, 2019
Wananchi wenye hasira kali wamemuua kisha kumchoma moto Juma Lugomba mwenye umri wa miaka 61, Mkazi wa Kijiji cha Chiwata Kata ya Chiwata Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara, baada ya Juma kudaiwa kumshambulia Mkewe kwa shoka na kumuua jambo lililosababisha Wananchi hao kupandwa na hasira na kumuadhibu.


Tukio hilo limetokea katika kijijini Chiwata, na limethibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Selemani Mzee ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya.

Mzee alisema inadaiwa juzi saa 3 usiku, Lugomba alimshambulia mkewe Yolenda Milanzi (59) na kitu chenye ncha kali na kumsababishia majeraha yaliyopelekea kifo baada ya kumjeruhi vibaya kichwani.

Alidai mkazi huyo baada ya kufanya mauaji hayo kwa mkewe, kundi la wananchi wenye hasira kali waliamua kumsaka na walipomkamata walimjeruhi kisha kumchoma moto hadi kusababisha kifo chake na yeye.

“Ni kweli tukio hilo limetokea mume kumshambulia mke wake na kumuua, lakini baada ya yeye kufanya mauaji hayo asubuhi yake wananchi waliamua kumsaka na walipomkamata walimjeruhi kisha kumchoma moto hadi kufa,” alieleza DC huyo.

Alisema bado chanzo cha mume huyo kufanya mauaji kwa mkewe hakijafahamika, lakini Polisi wanaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo.

Mtendaji wa Kijiji cha Chiwata, Thawabu Mturi alisema mume huyo baada ya kufanya mauaji, alikimbilia kijiji cha jirani cha Pemba kujificha ili kukwepa ushahidi.

Alisema wananchi walipogundua kuwa mume huyo amemuua mke wake, walipandwa na hasira ndipo walipoamua kumtafuta wakiwa na wamebeba silaha za kijadi na walipogundua kuwa amejificha katika kijiji jirani walifika huko na walifanikiwa kumkamata hivyo walimjeruhi kisha walimchoma moto hadi kufa.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post