WAZIRI MPINA AAGIZA MAENEO YALIYOTENGWA KWA AJILI YA WAFUGAJI KUPIMWA HARAKA


Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina, amewagiza watendaji wa sekta ya ufugaji kuhakikisha maeneo yote yaliyotengwa kwa ajili ya wafugaji kuhakikisha yanapimwa haraka na kuingiza mifugo ili kuondokana na migogoro ya wafugaji na wakulima. 


Waziri Mpina ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati wa kikao tathmini na watumishi wa wizara hiyo walioketi kutathmini mpango mkakati mpya wa mwaka wa fedha 2019¬2020. 


Amesema ni lazima maeneo yote yaliyotengwa yenye ukubwa wa hekta 350 na hekta laki mbili zilizotengwa na baadhi ya halmashauri kwa ajiri ya malisho wahakikishe yamepimwa ili kuepukana na migogoro  isiyo ya lazima katika maeneo mbalimbali hapa nchini. 


Aidha amesema ili kuondoa mikanganyiko ya kanuni wamefanya marekebisho ya kanuni ambapo halmashauri zote watatumia kanuni moja, tofauti na hapo mwanzo ambapo kila halmashauri ilikuwa na kanuni zake. 


Pia amesema kwa kipindi tangu ameingia katika Wizara hiyo wamejitahidi kwa  kupunguza migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji iliyokuwa imekithiri hapa nchi na mpaka sasa imepungua kwa kiasi kikubwa. 


Waziri Mpina pia amezitaka taasisi zilizochini ya wizara hiyo ikiwamo TVRA, NARCO na TARIRI, kuhakikisha zinajijenga na kujitegemea bila kutegemea ruzuku ya serikali, ili hizo ndio zitoe gawio kwa serikali. 


Kwa upande wake katibu mkuu wa Wizara hiyo, sekta ya Mifugo Prosefa Elisante Ole Gabriel, amesema katika kikao hicho wamawaambia watumishi ya Wizara hiyo matarajio ya serikali kwa wizara hiyo, na kuwataka kila sekta ihakikishe inatoa gawio kwa serikali.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post