WAZIRI LUGOLA AIPONGEZA JKT UJENZI NYUMBA ZA ASKARI MAGEREZA UKONGA | MALUNDE 1 BLOG

Monday, July 22, 2019

WAZIRI LUGOLA AIPONGEZA JKT UJENZI NYUMBA ZA ASKARI MAGEREZA UKONGA

  Malunde       Monday, July 22, 2019
 Na Felix Mwagara, MOHA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amesema ameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba za askari magereza unaofanywa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Ukonga jijini Dar es Salaam.

Waziri Lugola amesema Jeshi hilo linastahili pongezi kutokana na kasi ya ujenzi wa nyumba hizo ambao umefikia asilimia 70 kukamilika.

Akizungumza mara baada ya kumaliza ukaguzi wa ujenzi huo, Lugola amesema, atazungumza na Rais John Magufuli ili aweze kutoa kiasi cha fedha kilichobaki kwa ajili ya kukamilisha asilimia thelathini zilizobaki ili mradi huo ukamilike.

Lugola amesema, Jeshi la Kujenga Taifa lilikabidhiwa mradi huo zaidi ya miezi miwili iliyopita kutoka kwa Wakala wa Majengo (TBA) kufuatia agizo Rais Dkt. John Magufuli baada ya kuonekana kusuasua kwake.

Waziri Lugola amesema, amefurahia kuona ujenzi huo ukiendelea vema na kwa kasi kubwa na kuwapongeza askari hao kwa kazi kubwa wanayoifanya na kusisitiza kuwa anataka kuona zaidi kauli ya Mkuu wa Ujenzi huo akisema Jeshi halishindwi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu, alisema amefurahishwa na kasi hiyo, na ana uhakika JKT ipo vizuri na matumaini yake makubwa ujenzi huo utakamilika hivi karibuni.

Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Phaustine Kasike, amesema kukamilika kwa ujenzi huo kutawezesha jumla ya familia 172 za askari Magereza kuishi eneo katika makazi hayo huku ujenzi huo ukikadiriwa mpaka sasa kutumia zaidi ya shilingi bilioni.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post