Picha : MWANDISHI WA HABARI ASHEHEREKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA KWA KUWAPA ZAWADI WALIOJIFUNGUA HOSPITALI YA MKOA WA SHINYANGA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, July 23, 2019

Picha : MWANDISHI WA HABARI ASHEHEREKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA KWA KUWAPA ZAWADI WALIOJIFUNGUA HOSPITALI YA MKOA WA SHINYANGA

  Malunde       Tuesday, July 23, 2019

Mwandishi wa habari wa kituo cha matangazo Radio Faraja FM Stereo iliyopo Shinyanga Mjini Josephine Charles, amesheherekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutoa zawadi kwa wazazi ambao wamejifungua kwa njia ya upasuaji kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.


Tukio hilo limefanyika leo Julai 23, 2019 ambapo ni siku yake ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka kadhaa hapa duniani, ambapo ametembelea kwenye wodi ya wazazi ambao wamejifungua kwa njia ya upasuaji, wodi ambayo na yeye alijifungua mtoto wake Desemba 23,2018 kwa njia hiyo Christian Alex ambaye ametimiza miezi saba sasa.


Zawadi alizotoa kwa akina mama hao ni taulo za kike, sabuni za kufulia, kuogeshea watoto pamoja na poda, huku akitoa wito kwa wanawake kujenga utamaduni wa kuhudhuria kliniki mapema na kwa wakati pamoja na kujifungulia watoto wao kwenye huduma za kiafya mahali ambapo ni salama kuliko majumbani.

“Nimeamua kusheherekea siku yangu ya kuzaliwa kwenye wodi hii ya wazazi waliojifungua kwa njia ya upasuaji, wodi ambayo na mimi nilijifungua mtoto wangu kwa njia hii, ili kutoa hamasa kwa akina mama kupenda kujifugulia kwenye vituo vya afya na kuweza kupunguza tatizo la vifo vya mama na mtoto vitokanavyo na uzazi mkoani Shinyanga,” amesema Charles.

“Nasema haya kwa sababu siku ambayo mimi nililazwa kwenye wodi hii kwa ajili ya kujifungua mtoto wangu, alikuja mama mmoja akiwa hoi ambapo alipohojiwa ili kuchukuliwa taarifa zake aligundulika hakuwahi hata siku moja kuhudhuria kliniki, na alipozidiwa ndipo akaona aje hospitali kupatiwa huduma kitendo ambacho ni hatari kwa maisha yake,”amesema Charles.

"Pia natoa wito kwa watu wengine ambao wana nafasi wasiwe wanasheherekea siku zao za kuzaliwa kwa kufanya vitu vya anasa, bali wawe wanatumia fursa hiyo kusaidia watu ambao wana uhitaji ili na wao wasione kama jamii inayowazunguka imewatenga",ameongezaCharles.


Nao baadhi ya wazazi waliojifungua watoto wao kwa njia hiyo ya upasauaji akiwemo Dotto Jumanne na Winfrida Joseph ambao ni wakazi wa mkoani Shinyanga, wameshukuru kupewa zawadi hizo huku wakipongeza huduma ambayo wanapatiwa hospitalini hapo, ambapo wameweza kujifungua watoto wao salama.


Kwa upande wake Daktari wa wodi hiyo ya akina mama wanaojifungua kwa njia ya upasuaji Dkt. Amoni Amoni, alitoa wito kwa wadau wa afya mkoani humo kuendelea kutoa elimu kwa wakina mama juu ya umuhimu wa kuhudhulia Klinik mapema na kwa wakati pamoja na kujifungua watoto kwenye huduma za kiafya.

Na Marco Maduhu - Malunde1 blog

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI

Mwandishi wa habari kutoka kituo cha matangazo Radio Faraja Shinyanga Mjini Josephine Charles akizungumza nje ya wodi ya wazazi ambao wamejifungua watoto kwa njia ya upasuaji kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga, mara baada ya kumaliza kutoa zawadi kwao ikiwa ni siku ya kusheherekea siku yake ya kuzaliwa leo Julai 23,2019. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog

Mwandishi wa habari wa kituo cha matangazo Radio Faraja Shinyanga Mjini Josephine Charles (kwanza kushoto) akiwa na wanafamilia, waandishi wa habari wa Radio Faraja pamoja na baadhi ya wauguzi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga wakifungua zawadi kwa ajili ya kuwapatia wazazi.

Josephine Charles akitoa zawadi kwa wazazi ambao wamejifungua kwa njia ya upasuaji kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga wakati wa kusheherekea siku yake ya kuzaliwa, wodi ambayo na yeye alijifungua mtoto wake kwa njia hiyo ya upasuaji.

Josephine akiendelea kutoa zawadi.

Josephine akiendelea kutoa zawadi kwa akina mama waliojifungua watoto kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga kwa njia ya upasuaji.


Josephine akiendelea kutoa zawadi.

Josephine akiendelea kutoa zawadi kwa akina mama walijifungua watoto wao kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga , ikiwa anasheherekea siku yake ya kuzaliwa.

Zawadi zikiendelea kutolewa.

Josephine akiendelea kutoa zawadi huku akiwa amembeba mtoto wake Christian Alex ambaye alijifungua kwenye wodi hiyo kwa njia ya upasuaji.

Josephine akitoa pia zawadi kwa wauguzi wa wodi ya wazazi wanaojifungua kwa njia ya upasuaji kwa kutoa huduma nzuri na kuhakikisha wazazi wanajifungua salama na kupunguza vifo vya uzazi.

Mzazi Dotto Jumanne akishukuru zawadi hizo ambazo zimetolewa na Josephine Charles katika siku yake ya kuzaliwa.

Daktari wa wodi ya akina mama ambao wanajifungua wa njia ya upasuaji Dkt Amon Amoni, akitoa wito kwa akina mama kuhudhuria kliniki mapema na kwa wakati pamoja na kujifungulia kwenye huduma za kiafya, sabambamba na elimu itolewe zaidi kwa akina mama juu ya umuhimu wa kujifungulia kwenye huduma za afya mahali ambapo ni salama.

Dkt. Justice Minofu mwenye shati jekundu akimpatia zawadi ya siku yake ya kuzaliwa Josephine Charles ambaye amefikisha miaka kadhaa hapa duniani na kumtakia maisha mema na marefu.

Awali Josephine Charles akiwa na wafanyakazi wenzake wa Radio Faraja wakiwasili kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kutoa zawadi kwa wazazi ikiwa ni siku ya sherehe yake ya kuzaliwa.Kushoto ni Steve Kanyefu akifuatiwa na Joseph Edward.

Josephine Charles akipiga picha na familia yake, waandishi wa Radio Faraja na wauguzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga ,katika wodi ya wazazi waojifungua kwa njia ya upasuaji wakati wa kusheherekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutoa zawadi mbalimbali kwa wazazi hao.

Josephine Charles akipiga picha ya pamoja na familia yake, waandishi wa Radio Faraja na baadhi ya wauguzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga ,katika wodi ya wazazi waojifungua kwa njia ya upasuaji wakati wa kusheherekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutoa zawadi mbalimbali kwa wazazi hao.

Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post