WANANCHI 144 JIJINI DODOMA WAKABIDHIWA HATIMILIKI KWA MASHARTI NAFUU | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, July 31, 2019

WANANCHI 144 JIJINI DODOMA WAKABIDHIWA HATIMILIKI KWA MASHARTI NAFUU

  Malunde       Wednesday, July 31, 2019

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi amekabidhi hati ya viwanja kwa wananchi 144 wa Kata ya Tambukareli ambao maeneo yao yalitwaliwa na Serikali.


Kunambi amekabidhi hati hizo leo Julai  31,2019  kwa wananchi hao ambao wamekuwa wakihangaika takriban miaka mine hadi sasa. 


 Kunambi amefafanua kuwa  Halmashauri ya Jiji la Dodoma itahakikisha kila Mwananchi anapata haki yake kama ambavyo Rais Dk John Magufuli amekuwa akisisitiza kuwatetea wanyonge.

” Leo hii hapa kuna zoezi la kutoa viwanja kwa wananchi ambao ni wahanga wa maeneo yao ambao awali inadaiwa yalitwaliwa na iliyokua mamlaka ya ustawishaji Makao makuu na kuwaacha ndugu zetu hawa wakiwa hawana maeneo.

” Kwa muda mrefu kumekua na malalamiko ya muda mrefu ya wananchi na sisi kama Jiji tulifanya tathimini ya jumla na kuona ndugu zetu hawa wana haki ya kulipwa fidia maeneo yao na hivyo leo tumemaliza kero yao ya muda mrefu kwa kuwagaia viwanja bure na watakacholipia wao ni zile tozo za kawaida za kikatiba,” amesema Kunambi. 


Kunambi amesema katika mwaka  2018 wa Fedha tayari wameshatoa hati miliki 5000 na kuwa Jiji la kwanza Nchi nzima ikifuatiwa na Ilemela jijini Mwanza
.
” Ili tuweze kumaliza matatizo yote Dodoma basi Jiji linapaswa kutoa viwanja kwa mtindo huu wa leo kwa viwanja 5000 ambavyo vitatugharimu Shilingi Bilioni nne kwa hali ya kawaida sawa na kujenga vituo    vya afya 8. 


” Leo hii hawa wananchi ambao wako 144 tumewapa viwanja bure kwa maana watalipa tu zile gharama za kisheria takribani laki saba kwa kiwanja ambacho angeweza kulipa Shilingi Milioni saba. Hii ni kuonesha jinsi gani Serikali ya Dk Magufuli inatetea haswa wanyonge,” amesema Kunambi. 


Hata hivyo Kunambi amesema badala  ya Mwananchi kutoa gharama ya Tsh. milioni saba  anapunguziwa na kutoa  Laki saba pekee  kwa kiwanja na utoaji wa fedha hizo ni kwa masharti nafuu kutoa kwa awamu ndani ya miezi 6.

Kwa upande wake Diwani wa Kata hiyo, Juma Mazengo akizungumza kwa niaba ya madiwani    jiji la Dodoma amemshukuru Mkurugenzi wa Jiji kwa namna alivyolivalia njuga suala lao na kuweza kumaliza kero ya wananchi wake ambao wameteseka kwa miaka minne.

” Nimshukuru Mhe Rais kweli tumeona jinsi gani anatetea wanyonge. Hii inaonesha jinsi gani anaziishi ahadi zake alizowaahidi wananchi wakati wa kampeni, tunayo furaha sana na hakika tumeona heshima tuliyopewa na Serikali yetu,”amesema Mhe. Mazengo.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post