WAFUGAJI NJOMBE WAULALAMIKIA UONGOZI WA KIWANDA CHA MAZIWA | MALUNDE 1 BLOG

Friday, July 19, 2019

WAFUGAJI NJOMBE WAULALAMIKIA UONGOZI WA KIWANDA CHA MAZIWA

  Malunde       Friday, July 19, 2019
Na. AMIRI KILAGALILA-NJOMBE

Licha ya jitihada kubwa zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais DR.John Pombe Joseph Magufuli ya kuhakikisha inatimiza ndoto za kuifikia Tanzania yenye uchumi wa viwanda, huko mkoani Njombe wafugaji wa vijiji vya kilenzi na Uwemba wameulalamikia uongozi wa kiwanda cha maziwa Njombe kwa kukwamisha maendeleo yao.

Wafugaji wa kijiji cha kilenzi wakizungumza na MPEKUZI wamesema wanakosewa haki kwa kupata malipo yao kwa muda usio mwafaka ukilinganisha na muda waliopeleka maziwa katika kiwanda hicho.

“Nina masikitiko kwamba kiwanda kinakokwenda sio kwenyewe kwasababu wakati wapo wale weupe kiwanda kilikuwa kinaenda vizuri sana,lakini pengine viongozi wetu wanamsikilizaje Rais wetu?, yaani badala ya kiwanda kukisimamia vizuri ili kiwasaidie wananchi hilo hakuna” wamesema Ditrick Mlyuka na Azakia Ndawala wafugaji

Aidha baadhi ya wafugaji wa kijiji cha Uwemba wameonyeshwa kusikitishwa na kiwanda hicho kutoa bei mbili tofauti.

“Tuna masikitiko makubwa sana kwa kuwa utakauta kiwanda kimoja kinatoa bei mbili,kwa mfano kijiji cha utalingolo wanapewa shilingi mia saba kwa lita,sisi hapa uwemba tunapewa shilingi mia tano sitini nayo tunapata sio kwa muda muafaka yaani karibu vipindi vitatu”wamesema wananchi

Kwa upande wake meneja wa kiwanda cha maziwa Njombe ndg.Edwirn kidehele amekiri kucheleweshwa kwa malipo kwa wafugaji hao.

“Malipo tumeanza kulipa lakini mfumo mzuri wa kulipa vizuri nafikiri mpaka mwishoni mwa mwezi huu wa saba,hiyo mifumo yote itakuwa vizuri, sasa hivi tumeanza kupata oda kubwa kwa hiyo mzunguko wa fedha utakuwa mkubwa”alisema Kidehele

Kipaumbele cha Serikali ya awamu ya tano ni kuona tunafikia Tanzania ya viwanda vivyo hivyo kwa wafugaji hawa wanasema kwamba wanatamani kuwa mchango mkubwa wa kuifikia Tanzania ya viwanda, lakini wanasema endapo tatizo hili lisipotatuliwa huenda viongozi wa viwanda wakawa ndio chanzo cha kutofikia lengo la serikali.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post