TUNDU LISSU AFUNGUKA SABABU YA KUTOMWANDIKA BARUA SPIKA WA BUNGE, JOB NDUGAI | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, July 2, 2019

TUNDU LISSU AFUNGUKA SABABU YA KUTOMWANDIKA BARUA SPIKA WA BUNGE, JOB NDUGAI

  Malunde       Tuesday, July 2, 2019
Aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ameeleza sababu ya kutomwandika barua spika wa Bunge, Job Ndugai kumjuliusha kuwa yupo nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.


Wiki iliyopita Spika Ndugai alitangaza kumvua ubunge Lissu kwa kile alichoeleza kuwa kiongozi huyo hajulikana halipo zaidi ya kuonekana nchi za Ulaya na Marekani.

"Ni kweli sijawahi kumuandikia Spika Ndugai barua yoyote kuhusu mahali nilipo, na hali yangu ya kiafya. Sikumwandikia, sio kwa sababu nilisahau au nilipuuza, bali ni kwa sababu Spika Ndugai alikuwa anafahamu fika mahali nilipo, na sababu za mimi kuwa huko," amesema Tundu Lissu.

Ameendelea kwa kusema, "Kwa sheria na taratibu za Bunge, Spika na watendaji wake wanawajibika kufuatilia hali ya mbunge anayetibiwa nje ya nchi, na kutoa taarifa za maendeo yake. Sio wajibu wa mbunge mgonjwa kulitaarifu Bunge juu ya afya yake. Ndugai alipaswa kujua nilipo, na maendeleo yangu." Lissu,".


Aidha, Tundu Lissu amesema licha ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kudai hakujaza fomu za mali na madeni za viongozi wa Umma bado ana sifa za kugombea nafasi yoyote ya uongozi.

"Ili upoteze sifa ya kugombea ubunge au urais sharti uwe na hatia, sasa mimi sijakutwa na hatia na mahakama au mahakama ya Sekretarieti ya maadili, Ndugai peke yake hawezi kunitia hatiani bila kunisikiliza."

"Kwa hiyo mimi naweza kugombea nafasi yoyote ya uongozi iwe ubunge au urais. Kama wanataka nisigombee wanipeleke mahakamani au kwenye mahakama ya sekretarieti na wakiniuliza kwa nini sijajaza fomu nitawaambia nitawezaje kujaza nikiwa nje ya nchi," amesema Lissu

Amesema fomu hizo zinapaswa kujazwa na kuziwasilisha kwa njia ya mkono lakini zinapaswa kusainiwa na wakili wa Tanzania, "Sasa mimi niko hospitalini Ubelgiji, nawezaje kuzijaza, huku nampata wapi wakili, nawezaje kuzipeleka kwa mkono? Kwa hiyo walipaswa kuniuliza kwa nini sijajaza na si kuzungumza sijajaza bila kuwa na sababu."


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post