SAFARICOM YAMTEUA MICHAEL JOSEPH KUKAIMU NAFASI YA MTENDAJI MKUU ALIYEFARIKI JANA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, July 2, 2019

SAFARICOM YAMTEUA MICHAEL JOSEPH KUKAIMU NAFASI YA MTENDAJI MKUU ALIYEFARIKI JANA

  Malunde       Tuesday, July 2, 2019
Kampuni ya Safaricom imemteua ofisa mtendaji mkuu wake wa zamani, Michael Joseph kukaimu nafasi ya mtendaji mkuu iliyoachwa na Bob Collymore aliyefariki dunia jana Julai 1, 2019.
Kwenye mkutano maalumu wa wakurugenzi jana Jumatatu, bodi ya kampuni imeamua kumteua Michael Joseph kuongoza ambapo utekelezaji unaanza mara moja.
“Joseph atashikilia wadhifa huo hadi pale kampuni itakapotoa tangazo jingine kuhusu uteuzi wa kudumu,” Safaricom ilisema kwenye taarifa yake.
Joseph ni mjumbe katika bodi ya Safaricom na ni mwenyekiti wa sasa wa Shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways.
Mwili wa Collymore aliyechukua wadhifa huo kutoka kwa Joseph Novemba 2010, utazikwa leo jijini Nairobi katika tukio litakalohusisha tu wanafamilia.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post