RAIS KENYATTA UHURU KENYATTA AMALIZA ZIARA MKOANI GEITA NA KUREJEA KENYA


Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amerejea nchini kwake  baada ya kumaliza ziara ya siku mbili Tanzania.

Kenyatta ameondoka katika Uwanja wa Ndege wa Chato jana  mchana akisindikizwa na mwenyeji wake Rais wa Tanzania, John Magufuli.

Rais Kenyatta aliwasili Chato  Ijumaa ikiwa ni ziara yake binafsi baada ya kualikwa na Rais Magufuli.

Mara baada ya kuwasili alizungumza na wananchi akisisitiza umoja katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ili kuendeleza ushirikiano.

Pamoja na mambo mengine, kiongozi huyo alimjulia hali mama mzazi wa Rais Magufuli, Suzana.Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post