RAIS MAGUFULI AVITANDIKA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA TANZANIA...APONGEZA VYA KENYA

Rais Dk John Magufuli amevishangaa vyombo vya ulinzi na usalama kwa kushindwa kukamata dhahabu na fedha zilizoibiwa hapa nchini hadi zikakamatwa na vyombo vya ulinzi na usalama vya Kenya.


Magufuli amevihoji vyombo hivyo leo Jumatano Julai 24, wakati wa makabidhiano ya dhahabu iliyokamatwa nchini Kenya na kuwasilishwa  na Mjumbe Maalum wa Rais Kenyatta yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

“Wakupongezwa kwa hili ni vyombo vya ulinzi na usalama vya Kenya, najua wakuu wa vyombo Tanzania mpo hapa, lazima niwatandike hapa mbele za watu, kwasababu vitu vimetoka Mwanza vimekamatiwa Kenya, je zilipobebwa Mwanza na Kilimanjaro vyombo vyetu vilikuwa vinafanya nini?

“Je vilishirikiana na huyu muhalifu au vilimuachia, je dhahabu ngapi zimesafirishwa bila watuhumiwa kushikwa? Hili nawaachia nyinyi, mnafanya kazi nzuri ila inawezekana kuna mahali hamfanyi kazi vizuri nahii inadhihirisha aibu kwa vyombo vyetu na niwaombe mshirikiane, kila mtu asifanye kivyake.

 “Na mimi nitaandika barua rasmi ya kuvipongeza vyombo vya ulinzi na usalama vya Kenya kwa niaba ya Watanzania kwasababu wamefanya kazi nzuri kama wasingezikamata hizi mali leo tusingekuwa hapa, askari walioshiriki katika hili nitafanya mpango nione namna ya kuwazawadia wakiwa hukohuko Kenya,” amesema Rais Magufuli.

Chanzo - Mpekuzi blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527