RAIS MAGUFULI : SIWEZI KUTAWALA KWA KUONEA WATU WANYONGE

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameagiza Wizara ya katiba   na sheria kuendelea kupitia Magereza yote nchini ili kuweza kuwaachia wafungwa wasiostahili kifungo.

Rais Magufuli ametoa maelekezo hayo  Julai 18,2019  wilayani Kongwa   mkoani Dodoma wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara.

Mhe.Magufuli amesema baadhi ya wafungwa wamekuwa wakifungwa kwa kusingiziwa hivyo ni wakati sasa Umefika Kwa  Wizara kupita  kila gereza na kuchunguza uhalali wa kifungo ili kila mtu apate haki yake kwani serikali ya awamu ya tano ni Wanyonge.

Hivyo ,Rais Magufuli amesema serikali yake hawezi kutawala  kwa kuonea watu  wanyonge huku pia akisisitiza  Umuhimu wa viongozi  wa dini kuliombea taifa la Tanzania .

Katika hatua nyingine Rais Magufuli amekumbusha Umuhimu wa  kufanya kazi kwa bidii huku akisema asiyefanya kazi na asile na Serikali yake haiwezi kugawa chakula kwa mtu Mzembe.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527