RAIA WA HUNGARY AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUKUTWA NA DAWA ZA KULEVYA | MALUNDE 1 BLOG

Friday, July 26, 2019

RAIA WA HUNGARY AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUKUTWA NA DAWA ZA KULEVYA

  Malunde       Friday, July 26, 2019
Raia wa Hungary Akos Berger (28), amepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashitaka ya kusafirisha dawa za kulevya zenye uzito wa gramu  250  aina ya Amphetamine.


Berger amefikishwa mahakamani hapo  Juali 25,2019 na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Maira Kasonde.

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali, Grory Mwenda amedai,  Julai 19 mwaka huu, eneo la Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alitenda kosa hilo.

Hata hivyo, baada ya kusomewa mashitaka hayo, Hakimu  Kasonde alimtaka mshitakiwa kutojibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya dawa za kulevya, isipokuwa kwa kibali maalumu kutoka kwa DPP

Upande wa mashitaka ulidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilka na kesi iliahirishwa hadi Agosti 9 mwaka huu itakapotajwa.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post