PROFESA MBARAWA AKERWA NA WAKANDARASI WA MAJI WABABAISHAJI SHINYANGA, ALAZIMIKA KUWASAINISHA MAKUBALIANO MAALUM


NA SALVATORY NTANDU

Waziri wa Maji Prof, Makame Mbarawa amewaagiza wakandarasi wanaojenga mradi wa maji ya Ziwa victoria  kutoka kahama hadi  Isaka kwenda wa mkuu wa wilaya ya kahama kuandika makubaliano maalumu ambayo yataonesha ni lini watakamilisha miradi hiyo baada ya kushindwa kukamilisha miradi hiyo kwa wakati.

Uamuzi huo umetolewa jana na Prof.Mbarawa baada ya kupokea taarifa za kutokamilika kwa mradi huo kutokamilika kwa wakati huku wakiendelea kutoa ahadi za uongo.

Mbarawa amefafanua kuwa Wakandarasi hao wameshindwa kutimiza mashariti ya mkataba walioingia na serikali hivyo hawatakuwa na nafasi tena ya kuendendelea kutokamilisha mradi huo licha ya kuwa fedha wameshalipwa na serikali.

Amesema serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais, Dk John Magufuli haitakubali kuendelea kuwakumbatia wakandarasi wazembe ambao wanakwamisha shughuli za maendeleo ya wananchi katika maeneo wanayoishi.

Kwa upande wake Ezekiel Maige ni mbunge wa jimbo la Msalala amemuomba  Waziri Mbarawa kuwabana wakandarasi hao ili mradi huo ukamilike kwa wakati ili kuwawezesha wananchi kupata maji safi na salama.

Nao baadhi ya wananchi Kurwa Kitunga na Kashindye Singu  wa Kata za Mwakata na Mwendakulima waliojitokeza katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na Waziri huyo wameomba kujengewa magati ya maji katika vijiji ambavyo kunashida ya maji ili kuwawezesha kuacha kutumia maji ambayo sio safi yanayotumika pamoja na wanyama.

Kampuni zilipewa dhabuni ya kujenga mradi huo ni pamoja na Oriental conslin limited na Changs ambazo zimepewa kandarasi hiyo yenye thamani ya zaidi ya bilioni 22 ambapo walitakiwa kukamilisha mradi huo mwezi june  mwaka huu.

Bado Waziri Mbarawa anaendelea na ziara yake ya kikazi ya siku 4 mkoani shinyanga kukagua miradi mbalimbali ya maji.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post