POLISI DODOMA WADAI KUUA JAMBAZI SUGU


Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limedai kumuua kwa kumpiga risasi mtuhumiwa sugu wa ujambazi aliyefahamika kwa jina la Sostenes Muganyizi  maarufu Rasta aliyeuawa baada ya kujaribu kurushiana risasi na askari polisi katika mtaa wa Ubemebeni wilayani Kondoa ambapo inadaiwa jambazi huyo amefanya matukio ya kiuhalifu katika mikoa  mbalimbali hapa nchini na alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu.


 “Huyu ni jambazi sugu na kutokana na taarifa njema za raia zikatufikia, hii ni bunduki inayomilikiwa na Serikali na tukikuta mtu binafsi hasa jambazi anamiliki bunduki ya Serikali hakuapa kupewa na mkuu wa nchi ni lazima tumuondoe

“Sasa sadaka aliyoikusanya hapa anakwenda kula moto mbinguni, alikuwa na risasi kumi (10) ndani ya bunduki hii na akapiga tatu (3) saba zimebaki lakini yeye amelala, Askari wetu ni wepesi wanajua mbinu za kupambana na majambazi, watapata tabu sana," Amesema Kamanda wa Polisi Dodoma Gilles Muroto 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post