OLE SENDEKA ATOA AGIZO ZITO KWA WATENDAJI WANGING'OMBE

Na Amiri kilagalila-Njombe

Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka ameagiza kuchukulia hatua za kisheria kwa watendaji wote waliosababisha kuwapo kwa hoja katika ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG  katika mradi wa maji wa Igosi wilayani Wanging'ombe.

Katika mradi huo imeonesha kuwa zaidi ya shilingi milioni 100 zilishindwa kuokolewa na halmashauri ya Wanging'ombe kutokana na kumchukua mkandarasi wa gharama kubwa ya shilingi milioni 418 kuliko aliyekuwa na gharama ya chini ya shilingi milioni 279.

Agizo hilo amelitoa katika kikao maalum cha baraza la madiwani katika halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe cha kujadili taarifa ya mkaguzi wa hesabu za serikali ambayo imeonesha kuwapo kwa takribani hoja 11 zinazotakiwa kujibiwa kati ya hoja 40 ambazo 29 kati yake zimejibiwa.

“nataka muweke mambo wazi,kwa hiyo nataka kuona hatua zilizochukuliwa kwa wote waliohusika hakuna anayebaki dhidi ya waliosababisha hoja hizo,na msipoleta kwangu taarifa hiyo mimi nitachukua hatua dhidi ya wale ambao nina mamlaka nao”amesema Olesendeka

Onesmo lyandala ni diwani wa kata ya Imalinyi na Essau sanga ni diwani wa kata ya malangali ambao pia wamesema kuwa kitendo cha wao kutofahamishwa mradi huo na kufanyika kimya kimya inaashiria hakukuwa na uwazi na hivyo wameunga mkono agizo la mkuu wa mkoa juu ya kutakiwa kuchukuliwa hatua kwa maofisa waliohusika katika kuzalisha hoja ya CAG

“Sisi tunaone iko sawa kwasababu lazima watendaji wetu wote wafanye kazi kwa kufuata matakwa ya kisheria ,imefikia wakati watendaji wanafanya kazi kwa mazoea,na mwisho wa siku hoja zinakuja za jumla mpaka baraza la madiwani linahojiwa”wamesema baadhi ya madiwani

Pamoja na agizo hilo mwenyekiti wa hamlashauri ya wilaya ya Wanging'ombe Antony mahwata amesema hoja hiyo imetokana na maelekezo ya kitaalamu kutokana na uhalisia wa mradi wenyewe.

“wataalamu walimpa huyo darkadi kwa milioni 418 wakisema huyu walau amefika kwenye engenear estimate ambayo ilikuwa ni milioni 460 na hivyo angepewa mwingine wa milioni 279 angeshindwa kwasababu kulikuwa na BOQS zilizoandaliwa kitaalamu ili ule mradi uwe wa viwango vinavyotakiwa”amesema Mahwata
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post