WARSHA YA 4 KUPINGA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI KWA MKOA WA SHINYANGA YAFANYIKA JIJINI DODOMA


Mkurugenzi wa Maendeleo ya jamii kutoka Wizara ya Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto, Patrick Golwike,akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya tathimini khusu ndoa za utotoni iliyoitishwa na Shirika la Save the Children iliyofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi kutoka Save the Children Makao Makuu Dar es Salaam Bi.Angela Makota akitoa taarifa wakati wa ufunguzi wa warsha ya tathimini khusu ndoa za utotoni iliyoitishwa na Shirika la Save the Children iliyofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi Idara ya Watoto wizara ya Afya Sebastian Kitiku,akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya tathimini khusu ndoa za utotoni iliyoitishwa na Shirika la Save the Children iliyofanyika jijini Dodoma.
Mratibu wa ufuatiliaji wa Shirika la Save the Children, Kanuty Munishi,akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani)wakati wa ufunguzi wa warsha ya tathimini khusu ndoa za utotoni iliyoitishwa na Shirika la Save the Children iliyofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya wadau wakifuatilia wakati wa ufunguzi wa warsha ya tathimini khusu ndoa za utotoni iliyoitishwa na Shirika la Save the Children iliyofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya jamii kutoka Wizara ya Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto, Patrick Golwike,akiwa katika picha ya pamoja na viongozi kutoka Shirika la Save the Children na wadau mara baada ya kufungua warsha ya tathimini khusu ndoa za utotoni iliyoitishwa na Shirika la Save the Children iliyofanyika jijini Dodoma.
....................

Na.Mwaandishi wetu,Dodoma

Warsha ya nne ya tathimini na kupinga mila na desturi za mimba na ndoa za utotoni kwa mkoa wa Shinyanga imefanyika leo Julai 16,2019 Makao makuu ya nchi,jijini Dodoma.

Akizungumza katika warsha hiyo ya tathmini iliyokutanisha wadau mbalimbali wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga,Kaimu katibu mkuu wizara ya Afya,maendeleo ya jamii,jinsia Wazee na Watoto ,Idara kuu ya Maendeleo Patrick Golwike amesema lengo la warsha hiyo ni mpango mkakati wa kupashana habari na kupambana na mila potofu dhidi watoto .

Golwike ambaye pia ni mkurugenzi idara ya Maendeleo ya Jamii ametaja baadhi ya mila na desturi potofu na zenye madhara ambazo zimeshamiri mkoani Shinyanga ni mimba za utotoni , kumwozesha mtoto wa kike mapema kwa tamaa ya kupata ng’ombe huku akibainisha kuwa mkoa wa Shinyanga ukishika nafasi ya kwanza hapa nchini kwa asilimia 59% .

Aidha lengo la warsha hiyo ni kuelimisha jamii athari za ndoa Za Utotoni hususan Mkoani Shinyanga ambapo sheria mbalimbali zimewekwa katika kukabiliana na hilo.

Bw.Golwike amesema katika utafiti mdogo uliofanywa na Shirika la Save The Children mkoani Shinyanga ulibaini kuwa 90% ya wananchi wanafahamu kuwa ni kosa kumwozesha mtoto wa kike huku ikiamini kuwa kumwozesha mtoto mdogo inachochea na kuvutia kupata mahari nyingi zaidi mfano ng'ombe 25 hadi ng'ombe 50.

Hata hivyo,Bw.Golwike amesema mradi wa kuelimisha jamii juu ya maddhara ya ndoa za utotoni mkoani Shinyanga umefikia jumla ya watu Themanini na nne elfu [84 ,000]kwa wilaya za Ushetu na Kishapu kati ya watu thamanini na tano elfu [85,000]waliokusudiwa .

Kwa upande wake mdau wa elimu juu ya kupinga Mila potofu ,Paulo Robert kutoka Ukune Ushetu Mkoani Shinyanga amesema baada ya kupata elimu naye akaitumia vyema elimu hiyo kuelimisha watu wengine hususan Mimba na ndoa za utotoni.

Kwa Upande wao baadhi ya Wanafunzi waliohudhuria warsha hiyo wamesema wataendelea kupambana na ndoa za utotoni katika jamii wanayoishi.

Warsha hiyo imekutanisha asasi mbalimbali za kiraia ikiwa ni pamoja na SAVE THE CHILDREN,KIWOHEDE ,Umoja wa Ulaya,ambapo dhumuni kuu ni kuangalia changamoto za mimba na ndoa za utotoni hususan katika mikoa 6 ya Shinyanga,Tabora,Dodoma,Rukwa ,Manyara, na Katavi ambayo ndiyo mikoa inayoongoza kwa mila na desturi za ndoa za utotoni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527