Picha : WAZIRI MHAGAMA AFUNGUA WARSHA YA WADAU KUJADILI FURSA ZA BOMBA LA MAFUTA -EACOP SHINYANGA

Waziri Wa Nchi Ofisi Ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira Na Watu Wenye Ulemavu),Mhe. Jenista Mhagama amefungua warsha ya siku mbili ya majadiliano ya wadau kuhusu ushiriki wa Watanzania (Local content) katika sekta ya uziduaji mkoani Shinyanga. 

Warsha hiyo imewakutanisha pamoja wawakilishi 100 wa makundi mbalimbali kutoka mikoa 11 ili kujadili mikakati na maendeleo ya utekelezaji wa dhana ya ushiriki wa Watanzania katika mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima nchini Uganda kwenda Tanga, Tanzania na sekta ya madini kwa ujumla.

Akizungumza wakati wa kufungua warsha hiyo leo Jumatano Julai 3,2019 katika ukumbi wa Karena Hoteli Mjini Shinyanga, Mhe. Mhagama aliwataka viongozi wa maeneo ambako bomba litapita wawahamasishe wananchi kuchangamkia fursa zitakazokuwepo katika utekelezaji wa mradi huo na kujiletea maendeleo.

"Mradi wa EACOP ni moja kati ya miradi mikubwa ambao una manufaa mengi kwa nchi yetu katika kuzalisha Ajira, kuendeleza urithishaji wa ujuzi na teknolojia, ubia kati ya makampuni ya Tanzania na wageni, ununuzi wa bidhaa zinazozalishwa na kupatikana nchini, utoaji wa huduma za makampuni ya ndani, ushiriki wa jamii, ununuzi wa hisa kwa Serikali ya Tanzania na tozo za kodi.

 Hivyo, Watanzania tuna wajibu wa kuhakikisha tunashiriki ipasavyo kama ilivyo katika miradi ya sekta za ujenzi, madini na kadhalika",alisema. 

"Bomba hili la Mafuta lina urefu wa km 1443 kati ya hizo km 296 zipo nchini Uganda na km 1147 zipo Tanzania. Hii ni fursa kubwa kwa kuwa zaidi ya robo tatu ya Bomba litapita Tanzania na kunufaisha Watanzania",aliongeza Mhe. Mhagama.

Aliitaja mikoa nane itakayopitiwa na Bomba kuwa ni Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga huku akibainisha kuwa bomba litapita katika wilaya 24, Kata 134 na vijiji zaidi ya 180 na kusisitiza kuwa juhudi na jitihada za dhati zinapaswa kufanyiwa kazi ili kuwezesha ongezeko la ushiriki wa Watanzania.

Warsha hiyo imefadhiliwa na Taasisi ya Haki Rasilimali kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) PSF kwa kuzileta pamoja Asasi za Kiraia, wawakilishi wa jamii, wataalamu kutoka Wizarani, na Taasisi za Serikali,waratibu wa madawati ya uwezeshaji kutoka katika mikoa ya Shinyanga, Kagera, Geita, Mwanza, Mara, Singida, Manyara, Arusha, Tanga, Simiyu na Tabora ili kuwawezesha wadau hao na Watanzania kwa ujumla kufahamu maendeleo na fursa za sekta ya uziduaji. 
Na Kadama Malunde - Malunde1 blog

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Waziri Wa Nchi Ofisi Ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira Na Watu Wenye Ulemavu),Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga,Mhe. Gulam Hafeez Mukadam ambaye pia ni Mwenyekiti wa ALAT taifa wakati akiwasili katika Manispaa ya Shinyanga ili kufungua warsha ya siku mbili ya majadiliano ya wadau kuhusu ushiriki wa Watanzania (Local content) katika sekta ya uziduaji mkoani Shinyanga leo Jumatano Julai 3,2019. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack (aliyevaa ushungi) akimwongoza Waziri Wa Nchi Ofisi Ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira Na Watu Wenye Ulemavu),Mhe. Jenista Mhagama kuingia katika ukumbi wa Karena Hotel kwa ajili ya kufungua warsha ya siku mbili ya majadiliano ya wadau kuhusu ushiriki wa Watanzania (Local content) katika sekta ya uziduaji mkoani Shinyanga.
Meza kuu wakiongozwa na Waziri Wa Nchi Ofisi Ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira Na Watu Wenye Ulemavu),Mhe. Jenista Mhagama wakiimba wimbo wa taifa.
Waziri Wa Nchi Ofisi Ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira Na Watu Wenye Ulemavu),Mhe. Jenista Mhagama akizungumza wakati wa kufungua warsha ya siku mbili ya majadiliano ya wadau kuhusu ushiriki wa Watanzania (Local content) katika sekta ya uziduaji mkoani Shinyanga.
Waziri Wa Nchi Ofisi Ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira Na Watu Wenye Ulemavu),Mhe. Jenista Mhagama akizungumza wakati wa kufungua warsha ya siku mbili ya majadiliano ya wadau kuhusu ushiriki wa Watanzania (Local content) katika sekta ya uziduaji mkoani Shinyanga.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),Bengi Issa akizungumza wakati wa kufungua warsha ya siku mbili ya majadiliano ya wadau kuhusu ushiriki wa Watanzania (Local content) katika sekta ya uziduaji mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili ya majadiliano ya wadau kuhusu ushiriki wa Watanzania (Local content) katika sekta ya uziduaji mkoani Shinyanga.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Haki Rasilimali,Donald Kasongi akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili ya majadiliano ya wadau kuhusu ushiriki wa Watanzania (Local content) katika sekta ya uziduaji mkoani Shinyanga.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga,Mhe. Gulam Hafeez Mukadam akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo.
Wadau wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa warsha hiyo.
Wadau wakifuatilia matukio ukumbini.
Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu,Mhe. Nyabaganga Talaba akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack  wakati wa warsha hiyo.
Kushoto ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga,Mhe. Gulam Hafeez Mukadam akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Haki Rasilimali,Donald Kasongi na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),Bengi Issa wakiwa ukumbini.
Wadau wakiwa ukumbini.
Warsha inaendelea.
Wadau wakiwa ukumbini.
Warsha inaendelea.
Wadau wakiwa ukumbini.
Waziri Wa Nchi Ofisi Ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira Na Watu Wenye Ulemavu),Mhe. Jenista Mhagama  akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack  baada ya kufungua warsha ya siku mbili ya majadiliano ya wadau kuhusu ushiriki wa Watanzania (Local content) katika sekta ya uziduaji mkoani Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post