MEMBE KAKIRI SAUTI ILIYOVUJA NA KUSAMBAZWA MITANDAONI NI YA KWAKE


Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Bernard Membe, amesema sauti zilizovuja hivi karibuni kupitia mitandao ya kijamii ikihumusisha yeye akifanya mazungumzo na mtu asiyefahamika wakijadili juu ya sintofahamu ndani ya CCM ni ya kwake.

Membe ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na vyombo habari, ambapo amesema ni kweli sauti iliyodukuliwa na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii ni ya kwake asilimia 100 huku akiomba Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuingilia kati suala hilo.
 


"Sauti ni za kwangu, ni mimi 100 kwa 100 na nimeifanyia kazi na ninajua imetoka wapi kwa sababu nina miiko ya kuzingatia sisemi.

"Ni sauti ya kwangu kabisa na ninaelewa kila kilichotokea. Unaweza kuingia ugonjwa wa udukuzi, kama wale wanaotoa taarifa hizi za udukuzi hawachukuliwi hatua, 'hackers' (wadukuzi) wapo duniani, wanataka fedha tu.

"Ni kosa la jinai kudukua mawasiliano ndiyo maana dunia nzima huwasikii wanadukuana waziwazi. Hapa kwetu watu wenye wajibu wa kukataza udukuzi ni TCRA (Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano) mitandao yote ipo chini yao.

"Tuna sheria zipo, sheria mpya ya mwaka 2013, sidhani kama imerekebishwa, inakataza katakata udukuzi na dunia nzima hamuisikii ikifanya hayo ". amesema Membe.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527