KATIBU MKUU WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO DOTO JAMES AWATAKA WATUMISHI KUWAJIBIKA NA KUZINGATIA MAADILI YA KAZI


Na Josephine Majura, WFM, Dodoma
Watumishi wa Wizara ya Fedha ya Mipango wametakiwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma katika kutekeleza majukumu yao.


Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Doto James wakati wa kikao cha watumishi wa Wizara hiyo.

Bw. James alisema kuwa watumishi wote wanawajibu wa kufanya kazi kwa ufanisi na weledi na kwa kuzingatia nidhamu, maadili, sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa Umma.

“Ni wajibu wa kila mtumishi kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi  wote wanaohitaji huduma katika Wizara yetu” Alisema Bw. James.

Aidha Bw. James aliwapongeza Watumishi wa Wizara hiyo kwa kazi wanazozifanya hususan kazi ya uandaaji wa Bajeti Kuu ya Serikali iliyopishwa na Bunge hivi karibuni na kuwataka waendelee kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa Bajeti hiyo.

Kwa upande wa Watumishi wa Wizara hiyo waliupongeza uongozi wa Wizara hiyo kwa kutenga muda wa kuzungumza nao na kusikiliza changamoto mbalimbali zinazo wakabili pamoja na kuzitolea ufafanuzi.

Waliahidi kutatekeleza maelekezo yote aliyotolewa kwa uadilifu ili kuongeza ufanisi wa kazi kwa maendeleo ya nchi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post