BALOZI SOKOINE AFUNGUA MAFUNZO YA WAWEZESHAJI WA MASHAMBA DARASA | MALUNDE 1 BLOG

Monday, July 8, 2019

BALOZI SOKOINE AFUNGUA MAFUNZO YA WAWEZESHAJI WA MASHAMBA DARASA

  Malunde       Monday, July 8, 2019

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Balozi Joseph Sokoine leo amefungua Mafunzo ya Msasa ya Uwezeshaji kuhusu Mashamba darasa kwa Maafisa viungo wa mradi kutoka Wizara na timu za uwezeshaji za wilaya wa mradi wa kurejesha ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula katika maeneo kame nchini (ldfs), katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Morogoro.


“Ni matumaini yangu kuwa elimu na ufahamu mtakauopata kupitia mafunzo haya, mtaitumia katika kufanikisha uanzishaji wa mashamba darasa katika maeneo ya mradi” alisema Balozi Sokoine.

Mafunzo hayo ya siku 5 yanalenga kujenga uwezo kwa washiriki katika uanzishaji wa mashamba darasa katika vijiji na shehia ambako mradi wa LDFS unatekelezwa.

Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wamekuwa wakitekeleza miradi inayolenga kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo kwa kusogeza karibu teknolojia kwa wakulima. Lengo likiwa ni kuongeza usalama wa chakula na kuongeza kipato cha jamii. Mradi wa LDFS ambao umeandaa mafunzo haya ni mfano wa juhudi hizo za Serikali. Juhudi hizi zinahusisha uingizaji na matumizi ya teknolojia mpya ikiwemo matumizi sahihi ya mbolea, mbegu zenye ubora; uboreshaji wa nyanda za malisho; utoaji wa huduma za ugani na mafunzo kupitia shamba darasa. Juhudi hizi zote zina lengo la urejesha ardhi iliyoharibika ili iweze kuendelea kuzalisha mazao ya kilimo, mifugo na misitu.

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi huo wa LDFS Bw. Joseph Kihaule amesema mradi huo utajumuisha na uanzishwaji wa mashamba darasa 100.

Wawezeshaji wa mradi huo ni Shirika la Kilimo na Chakula Duniani (FAO), Chuo cha Kilimo cha Sokoine (SUA) na Wakala wa Taifa wa Mbegu za Miti Tanzania (TTSA) ambapo washiriki wa mafunzo hayo wametoka Wizara za Kilimo, Maliasili na Utalii, Maji, Mifugo na Uvuvi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Idara ya Mazingira, Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar. Aidha, washiriki wengine ni kutoka katika Halmashauri zinazotekeleza Mradi za Mkalama, Micheweni, Magu, Nzega na Kondoa, pamoja waalikwa rasmi Daktari Moses Temi na Bwana Charles Mjema.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post