POLISI WATAJA SABABU ZA KUMSHIKILIA MWANDISHI WA HABARI ERICK KABENDERA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, July 30, 2019

POLISI WATAJA SABABU ZA KUMSHIKILIA MWANDISHI WA HABARI ERICK KABENDERA

  Malunde       Tuesday, July 30, 2019

Kamanda Lazaro Mambosasa

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa amesema Jeshi la Polisi linamshikilia kwa mahojiano mwandishi wa habari Erick Kabendera aliyekamatwa Julai 29, 2019 nyumbani kwake maeneo ya Mbweni Jijini Dar es Salaam.

Kamanda Mambosasa amesema, mtuhumiwa huyo alikamtwa baada ya kukataa wito wa polisi ambapo awali aliandikiwa barua ya wito kwa ajili ya mahojiano, lakini alikaidi kutii wito huo na kusema kwamba, jeshi la polisi linapomuita mtu kwa hiari na akaacha kutii wito huo, hutumia mbinu ya kumlazimisha atii.

''Baada ya kukamatwa mwandishi huyo, tulisikia taarifa mbalimbali kutoka kwa kada mbalimbali kwenye jamii wakiendelea kusema mwandishi huyo alitekwa niseme kuwa, mwandishi huyo hakutekwa aliitwa, lakini kwa jeuri alikaidi kutii wito huo, sababu pia ya kuitwa ni kuhusiana na utata wa uraia wake, Jeshi linaendelea na upelelezi kwa kushirikiana na maafisa wa uhamiaji'', amesema SACP Mambosasa.

Aidha Kamanda Mambosasa ameongeza kuwa, baada ya upelelezi kukamilika jeshi hilo litahakikisha kosa analotuhumiwa nalo mwandishi huyo, linawekwa mezani ili na yeye aweze kuhakikishia kama ni mtanzania kwa kutoa vielelezo vinavyothibisha uraia wake.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post