JESHI LA POLISI DODOMA LANASA MTU MMOJA ALIYETAPELI KWA KUJIFANYA POLISI


Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Jeshi la polisi mkoani Dodoma limemshikilia  RAJAB RAMADHAN[32] aliejifanya  askari polisi  Kwa     kutapeli  watu  mbalimbali. 


Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake jijini Dodoma Leo Julai 23,2019 Kamanda wa polisi mkoani hapa Gilles  Muroto amesema kwa muda Mrefu kijana huyo anayeishi eneo la Area A Mjini Dodoma amekuwa akijipatia huduma mbalimbali kwa udanganyifu akijifanya askari polisi na kutishia watu kwa silaha  bandia. 


Kamanda Muroto ametaja vifaa alivyokuwa navyo  mhalifu huyo kuwa ni sare ya polisi Jangle Green,pistol ya bandia na hoster yake,picha akiwa na sare za jeshi [JWTZ] huku uchunguzi wa awali ukionesha kuwa kijana huyo alishawahi kuhudhuria mafunzo ya JKT na Kufukuzwa kwa utovu wa nidhamu. 


Katika hatua nyingine Kamanda Muroto amesema jeshi hilo limekamata  vifaa vya NIDA ambavyo ni kamera 12 ambapo mtumishi wa NIDA  Ezekiel Subugo [24] aliiba vifaa hivyo ofisini na kuwauzia watu  mitaani  na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani. 


Hata hivyo,Jeshi hilo limemkamata Musa Pungu akiwa na madawa ya kulevya aina ya Heroin kiasi  cha kete 132 zilizofungashwa katika vinailoni ambapo Kamanda Muroto amesema kijana Musa ameharibu vijana wengi kwa madawa ya kulevya katika Mtaa wa Hazina  jijini Dodoma hivyo mtuhumiwa na wenzake wanne watafikishwa mahakamani. 


Kamanda  Muroto ametoa wito kwa jamii kujihadhari na Matapeli katika jiji la Dodoma na hakuna Fedha zinazokuja kiurahisi bila kufanya kazi halali. 


Sanjari na hayo,Kamanda Muroto ameipongeza Kampuni ya INNOMAX kwa kulikabidhi jeshi hilo pikipiki mbili mpya aina ya HAOJUE na HONGLOG  zenye thamani ya zaidi ya Tsh.Milioni 4 Kwa ajili ya kufanyia doria  huku akiwaasa Watanzania wengine kuwa na uzalendo wa kusaidia jeshi hilo.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527