WAGANGA WA TIBA ASILI IRINGA WAPINGANA NA 'WAZEE WA GAMBOSHI' KUPOTEZA WATAKAOMPINGA MAGUFULI | MALUNDE 1 BLOG

Monday, July 29, 2019

WAGANGA WA TIBA ASILI IRINGA WAPINGANA NA 'WAZEE WA GAMBOSHI' KUPOTEZA WATAKAOMPINGA MAGUFULI

  Malunde       Monday, July 29, 2019

Mwenyekiti wa shirikisho la tiba asili mkoa wa Iringa ,Abdu Kisige amesema hawaungi mkono tamko la waganga wa jadi kutoka kijiji cha Gamboshi wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu kuwa watampoteza mwanachama yeyote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), atakayethubutu kuchukua fomu ya kugombea urais mwaka 2020 na kumpinga Rais John Magufuli.

Hivi karibuni Mwenyekiti wa Waganga wa Jadi mkoani Simiyu,Bwimila Shala alisema waganga wa jadi mkoani humo watahakikisha kuwa mwaka huu na mwaka unaokuja kwenye uchaguzi wanamlinda na yeyote yule atakayechukua fomu bila utaratibu wa waganga wa tiba asili watampoteza kwa njia yoyote ile.
Hata hivyo,Mwenyekiti wa shirikisho la tiba asili mkoa wa Iringa ,Abdu Kisige (pichani) leo amesema tamko hilo la waganga wa jadi kutoka Simiyu ni kinyume cha demokrasia.

"Waganga wa jadi Simiyu ni mashabiki wasiokuwa na demokrasia,wao wanatafuta tu wapendezwe,wanataka tu wapate sifa kwa rais,lakini ukweli hiyo siyo demokrasia na wala rais hawezi hayo kupendezwa nayo wala sisi watu wa Iringa hatukubaliani na hilo,sisi tunasema demokrasia ifanyike,anayetaka urais agombee,tatizo watu wengi wanashindwa kujua maana ya demokrasia,maana ya demokrasia siyo kulazimisha kila mtu atoe wazo lake", - Kisige
MTAZAME HAPA AKIZUNGUMZA

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post