VIWANDA VYA DAWA NA VIFAA TIBA KUJENGWA NCHINI

 Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwe akihutubia jijini Dar es Salaam jana kwenye mkutano wa kujadili namna ya kuanzisha viwanda vya dawa na vifaa tiba ulioandaliwa na Bohari ya Dawa (MSD) kwa ushirikiano wa Sekta binafsi na Umma (PPP) ambao uliwakutanisha wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali.

 Waziri wa Afya wa Tanzania, Ummy Mwalimu akizungumza kwenye mkutano huo.
 Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Mipango waMSD Bw. Sako Mwakalobo akizungumza kwenye mkutano huo.
 Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa meza kuu.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurean Bwanakunu akizunguma kwenye mkutano huo.

Na Mwandishi Wetu

VIWANDA vya dawa na vifaa tiba vinatarajiwa kujengwa hapa nchini na kuifanya Tanzania kutosheleza mahitaji ya soko la ndani.

Hayo yalibainishwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwe jijini Dar es Salaam jana kwenye mkutano wa kujadili namna ya kuanzisha viwanda hivyo kwa ushirikiano wa sekta binafsi na umma (PPP) ambao uliwakutanisha wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali.

Bashingwe alisema Serikali ya Tanzania imeandaa mazingira mazuri ya kuanzishwa kwa viwanda hivyo baada ya kuondolewa kwa kero kadhaa zilizokuwepo.

"Kero 54 zilizokuwa zikikwamisha uwekezaji huo zimeondolewa katika bajeti ya serikali ya 2019/2020 hivyo kuifanya Tanzania kuwa eneo bora la kuanzishwa kwa viwanda hivyo" alisema Bashungwe.

Waziri wa Afya wa Tanzania, Ummy Mwalimu akizungumza kwenye mkutano huo alisema tangu Serikali ianze kununua dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kutoka kwa wazalishaji imeweza kuokoa asilimia 40 ya fefha zilizokuwa zikitumika kununulia madawa kupitia kwa mawakala.

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurean Bwanakunu alisema mkutano huo umejenga ushirikiano mkubwa kati ya MSD na wadau wa sekta ya afya wakiwemo wazalishaji na wasambazaji.

Tanzania ilikuwa ni mwenyeji wa mkutano huo kwa ushirikiano wa MSD na PPP.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527