WAZIRI KAMWELWE KUWAPA NEEMA WATAALAMU WANAOSOMEA SEKTA YA ANGA

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe akizungumza wakati wa kufungua kongamano la pili la wadau wa sekta ya anga lililoandaliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania,(TCAA) Hamza Johari akizungumza wakati wa kongamano la pili la wadau wa sekta ya anga lililoandaliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) jijini Dar es Salaam.

Meza kuu...
Washiriki wakifuatilia kongamano.
Picha ya pamoja na wadhamini.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amesema yupo katika hatua za mwisho ya mazungumzo na Wizara ya Elimu ili itoe mikopo kwa wataalamu wanaosomea sekta ya anga.

Waziri Kamwelwe ameeleza hayo leo, wakati akifungua kongamano la pili la wadau wa sekta ya anga lililoandaliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).

Kongamano hilo, lina lengo la kujadili mafanikio na changamoto zinazoikabili sekta hiyo na mbalimbali zitawasilishwa ikiwemo mchango wa sekta ya anga kwenye ajenda ya kuipeleka Tanzania ya viwanda.

Kamwelwe ambaye pia mbunge wa Katavi (CCM) amesema tayari ameshazungumza na viongozi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) katika kufanikisha mchakato huo ili bodi hiyo ishiriki kikamilifu kuwasaidia wataalamu hao.

“Kulikuwa na hoja ya kwamba wataalamu hawa wanahitaji fedha nyingi, lakini nikawaambia hawa watalipa haraka kuliko hao wengine wanaokopeshwa. Nimeangalia vizuri hii fani rubani kufundishwa hadi kuiva ni fedha nyingi.”

“Hata mimi siwezi kumsomesha mwanangu kwa hizo fedha, hakuna namna kwa sababu tulishaamua kuikuza sekta hii. Lazima Serikali iingize mkono wake kama ilivyo kwenye mambo mengine,” amesema Kamwelwe.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527