WATUHUMIWA1842 WA MADAWA YA KULEVYA WATIWA MBARONI


  Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Mpaka kufikia  mwezi januari 2019 hadi  machi 2019 jumla ya makosa  113  dawa za kulevya yaliripotiwa  hapa nchini na watuhumiwa 1,842 wa makosa ya dawa za mirungi na bangi.

Hayo yamesemwa leo Juni 17,2019 bungeni jijini  Dodoma na Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni wakati akijibu swali la mbunge wa viti Maalum ,Zainabu Katimba aliyehoji serikali ya    awamu ya tano tangu iingie Madarakani  imebaini na kuwachunguza watu wangapi wanaojihusisha na mtandao wa dawa za kuleya. 


Katika majibu yake Yake,Mhandisi Masauni amesema tokea serikali ya awamu ya tano iingie Madarakani  imewabaini  makosa 679  na kuwakamata watuhumiwa  1,269 kwa mwaka 2016,Makosa 902, na watuhumiwa 1,578  mwaka 2017,Makosa 702 na watuhumiwa 886 kwa mwaka 2018 ,makosa 113 na watuhumiwa 1,842  kwa mwaka 2019. 


Aidha,Mhandisi Masauni  amesema madawa mashambani Mirungi na bangi yaliyokamatwa kwa mwaka 2016 ni  jumla ya makosa 10,375 na  watuhumiwa 26,031,makosa  8,956 na watuhumiwa 12,529 kwa mwaka 2017,makosa  7,539  na watuhumiwa 9,987 kwa mwaka 2018. 


Baadhi ya watuhumiwa  wamepelekwa mahakamani na wengine upelelezi wa Mashauri yao unaendelea huku Jeshi la polisi kupitia Programu ya kuzuia uhalifu limeendelea kutoa huduma ya urekebishaji kwa waathirika wa dawa za kulevya.

 
Kwa upande wake Waziri wa Ofisi ya Waziri mkuu ,vijana,ajira na watu wenye ulemavu Mhe.Jenista Mhagama amesema ofisi ya Waziri mkuu imefanikiwa kudhibiti dawa za kulevya kwa asilimia 95%  huku waathirika wote wa dawa za kulevya  wakipewa elimu pamoja na kufanya kazi ili kurejea katika hali yao ya kawaida.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527