THE DESK AND CHAIR FOUNDATION YAKABIDHI MIUNDOMBINU YA INTANETI KWA MPC


Mwenyekiti wa Taasisi ya "The Desk & Chair Foundation", Sibtain Meghji (kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza, Edwin Soko (kushoto) kifaa cha kusambaza mawasiliano ya mtandao wa Intaneti (Router) pamoja na nyaya za umeme (Cable) ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za chama hicho katika kutimiza vyema majukumu yake ya kihabari katika jamii.

Taasisi ya “The Desk & Chair Foundaton” ya jijini Mwanza imeunga mkono juhudi za Klabu ya Waandishi wa Habari ya Mkoa Mwanza (Mwanza Press Club-MPC) kwa kukabidhi miundombinu ya Intaneti.

Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Sibtain Meghjee amemkabidhi
Mwenyekiti wa MPC, Edwin Soko vifaa hivyo na kuahidi kuendelea kushirikiana bega kwa bega na klabu hiyo katika kuchochea maendeleo ya Mkoa Mwanza.

Baada yakupokea vifaa hivyo, Soko amesema uwepo wa miundombinu ya Intaneti ya uhakika kwa
waandishi wa habari ni nyenzo muhimu katika kutekeleza majukumu yao huku akiishukuru taasisi ya “The Desk & Chair Foundation” kwa mchango wake katika kuimarisha
shughuli za waandishi wa habari.

Katika hatua nyingine, Edwin Soko ameongeza kuwa MPC itaendelea kufanya kazi na taasisi ya The Desk & chair pamoja na wadau mbalimbali wa Mkoa Mwanza pamoja na Serikali ya awamu ya tano na kuchochea maendeleo ya Mkoa wa Mwanza.

“Uwezo wa miundombinu utasaidia waandishi wa habari kutuma habari zao na kupokea taarifa muhimu na pia kuhudhuria mikutano kwa njia ya mtandao” amesisitiza Soko.

Vifaa vilivyokabidhiwa ni kipanga njia cha Intaneti kimoja (Router), waya za kuunganishia kifaa hicho, waya za umeme pamoja na vifushi vya intanenti ambapo hatua hii imekuja baada ya MPC kupata uongozi mpya Juni 01, 2019 ambao umeanza kujenga mahusiano mema na wadau wa habari ili kujenga mahusiano mazuri.
Kifaa hicho (Router) kutoka kampuni ya mawasiliano Tanzania (TTCL) kina uwezo wa kuunganisha kompyuta 30 kwa wakati mmoja hivyo kitasaidia wanachama wa MPC kupata huduma ya intaneti kwa uhakika huku pia wasio wanachama wakichangia gharama kidogo za uendeshaji.

Via>>BMG  Habari

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527