TFDA YAKABILIANA NA SUMUKUVU KUPITIA MAABARA YA KISASA YA UCHUNGUZI WA CHAKULA


Na Grace Semfuko,MAELEZO
Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania TFDA imesema inayo maabara ya kisasa ya upimaji wa usalama wa mazao ya Chakula ili kuondokana madhara yatokanayo na ulaji wa vyakula vizivyopimwa yakiwepo magonjwa yanayotokana na ulaji wa vyakula vyenye Sumu kuvu.


Aidha Mamlaka hiyo imejipanga kupambana na magonjwa yanayosababishwa na ulaji wa vyakula hivyo ambayo yana athari kubwa kwa afya za binaadamu ikiwepo udumavu na vifo.

Hayo yalibainishwa na Mkaguzi wa chakula Mwandamizi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania TFDA Dkt Analice Kamala wakati akiwasilisha mada juu ya uchafuzi wa Sumukuvu madhara yake kwa afya na jinsi ya kudhibiti katika Semina ya kuwajengea uwezo Waandishi na Wahariri wa Habari katika kuelimisha jamii kuhusu usalama wa chakula iliyofanyika Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.

Dkt Kamala alisema alisema maabara za kisasa za upimaji wa vyakula zilizopo kwenye Mamlaka hiyo zina uwezo wa kisasa wa kubaini magonjwa au vimelea vya fangas ambavyo huathiri vyakula hususa vilivyohifadhiwa kwenye maeneo yasiyo salama ikiwepo sehemu ya  unyevu unyevu,joto na wadudu wa nafaka.

“ Niwahakikishie tu watanzania wenzangu kuwa vyakula vinavyopimwa kwenye maabara hii ni salama, hakuna kinachopita hapa kikiwa na madhara, kitatupwa tu, tuzingatie usalama wa vyakula na tutumie vyakula vilivyopimwa alisema Dkt Kamala.

Aidha katika hatua nyingine Dkt Kamala aliwataka Wanawake wanaonyoshesha nchini kuwa waangalifu katika uandaaji na matumizi ya vyakula wanavyotumia ili kuepukana na madhara ya Sumukuvu iliyopo kwenye baadhi ya vyakula vya nafaka ambayo inadaiwa kuwa na madhara kwa binaadamu na wakati mwingine husababisha vifo.

Dkt Kamala alisema iwapo Mama anayenyonyesha atatumia vyakula vyenye sumukuvu anasababisha madhara makubwa kwa Mtoto ikiwepo Udumavu, Vifo na Magonjwa ambayo yanaathiri ukuaji wa mtoto.

“Wanawake wanaonyonyesha ni muhimu kuzingatia uandaaji wa vyakula kwani watoto hula vyakula hivyo kupitia kwenye Maziwa ya Mama na hivyo kuathiri mfumo mzima wa ukuajiälisema Dkt Kamala.

Aidha pia Dkt Kamala alisema ulaji wa mazao ya mifugo iliyotumia vyakula vilivyoathiriwa na sumu kuvu pia inaweza kuathiri afya za binaadamu.

Alisema Sumu kuvu inaathiri ini na Figo na kusababisha ugonjwa wa manjano na wakati mwingine kuvuja damu kwenye maeneo ya wazi,kuharisha na kuhisi kichefuchefu na dalili zake huanza kuonekana baada ya wiki mbili.

Ugonjwa huo kwa Nchini Tanzania ulilipotiwa na Wizara ya Afya Juni 13 mwaka 2016 Mkoani Dodoma ambapo ilibainika kuwepo kwa watu 68 kwenye familia 42 kuugua magonjwa yatokanayo na ulaji wa vyakula vyenye sumu kuvu na kati yao watu 20 sawa na asilimia 30 walipoteza maisha.

Mwisho.
 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527