TANZANIA YAONGOZA KWA AMANI AFRIKA MASHARIKI

Tanzania imeongoza Afrika Mashariki kwa mujibu wa ripoti ya Global Peace Index (GPI) inayotolewa na taasisi ya uchumi na amani (IEP)yenye makao yake makuu mjini Sydney nchini Australia.


Tanzania imeshika nafasi ya 7 kwa kuwa nchi yenye amani kwa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara na duniani ikiwa imeshuka kutoka nafasi ya 51 mwaka 2018 hadi nafasi ya 54 mwaka 2019 kati ya nchi 163, huku Iceland, New Zealand, Uholanzi, Austria, Denmark, Canada, Singapore, Slovenia, Japan, na Jamuhuri ya Czech ni nchi zilizoorodheshwa kuwa na amani zaidi duniani.

Wakati Tanzania ikiongoza Afrika Mashariki, Rwanda imeifuata ikiwa ya pili Afrika Mashariki lakini imeshika nafasi ya 17 kwa nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara, ikifuatiwa na Uganda iliyoshika nafasi ya 23 , Kenya ya nne Afrika Mashariki na 28 katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara.

Nchi zilizoshika nafasi za juu katika eneo la jangwa la sahara ni Mauritius, Botswana, Malawi, Ghana, Zambia na Sierre Leone.

Kwa mujibu wa Ripoti hiyo, nchi zilizo na kiwango cha chini cha amani ni Burundi,Chad, Cameroon, Mali, Nigeria, DR Congo, Somalia na Sudani Kusini.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527