TAARIFA KUHUSU MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA


Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuwatangazia wananchi wote kuwa, itashiriki Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kuanzia tarehe 17 hadi 22 Juni 2019. Maadhimisho haya ni kwa mujibu wa kalenda ya Umoja wa Afrika (AU) ambapo nchi wanachama huadhimisha kwa kushiriki shughuli mbalimbali zinazohusu Utumishi wa Umma.


Wakati wa maadhimisho hayo, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeandaa madawati maalum ya kutoa huduma kwa wananchi katika Ofisi za Wizara zilizopo Kata ya Mtumba jijini Dodoma na zile zilizopo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Huduma zitakazotolewa ni pamoja na kusikiliza na kutoa ufafafanuzi wa hoja mbalimbali za wananchi kuhusu Wizara pamoja na kutoa elimu kuhusu majukumu yanayotekelezwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika.

Madawati hayo yatakuwa wazi kuanzia saa 1.30 asubuhi hadi saa 10.00 jioni.

NYOTE MNAKARIBISHWA.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
14 Juni 2019


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post