SIMBA SC YAMPIGA PINGU KAGERE


MFUNGAJI Bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Mnyarwanda mwenye asili ya Uganda, Meddie Kagere amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuitumikia klabu ya Simba.
Kama kawaida, Simba SC mchana wa leo imemtambulisha mchezaji iliyemsajili na kwa mara nyingine imeendelea kuwapa mikataba mipya wachezaji wake waliokuwepo kwenye kikosi cha msimu uliopita.

Uamuzi wa Simba kumuongezea mshambuliaji wake Meddie Kagere miaka
Miwili umeelezwa umetokana na mambo mawili makubwa.

MOJA:
Ni baada ya Kagere raia wa Rwanda kufanya vema msimu uliopita akiibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara. Hivyo Simba wameona makali yake bado wanayahitaji.


MBILI:
Simba imeona idadi ya timu zinazomfuatilia Kagere kutaka kupata saini yake zimeongezeka.


Hadi timu kubwa kama Al Ahly, Zamalek nazo zimeonyesha nia na Simba walichofanya ni kumpa mkataba na baada ya hapo ni tusubiri atakayemtaka amwage mamilioni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527