SERIKALI YAPATA DOLA ZA MAREKANI MILIONI 500 KUTOKA INDIA KWA AJILI YA KUTEKELEZA MIUNDOMBINU YA MAJI


Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
Serikali imepata fedha kutoka serikali ya india kiasi  cha dola za marekani milioni 500 kwa ajili ya kuboresha huduma ya miundombinu ya maji  katika miji 28 ya Tanzania na Zanzibar.
 

Hayo yamesemwa leo Juni 19,2019  bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso  wakati akijibu swali la mbunge wa Kilombero,Peter Lijualikali  aliyehoji,serikali ina mpango gani wa kuongeza mtandao wa Maji.


Akijibu Swali hilo,Naibu waziri wa maji Mhe.Aweso amesema Katika mpango wa Muda Mrefu,serikali imepata fedha kutoka serikali ya India kiasi  cha Dola za Marekani Milioni 500 kwa ajili ya kuboresha huduma ya miundombinu ya maji katika miji 28 ya Tanzania bara  na Zanzibar ambapo mji wa Ifakara ni miongoni mwa miji itakayopata maji kupitia fedha hizo na sasa taratibu za kuwapata wataalam washauri watakaofanya usanifu  wa kina na maandalizi ya makabrasha unaendelea.

Hata hivyo ,Mhe Aweso amesema kukamilika kwa mipango hiyo kutaboresha hali ya upatikanaji wa Maji kwa asilimia 90%.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post