Serikali kutoa matibabu ya Sickle cell (Seli mundu) Bure

Serikali imesema imeandaa mpango wa kutoa matibabu ya bure kwa watoto watakaokuwa wakiugua ugonjwa wa Selimundu, kwa kupatiwa vibali maalum vya huduma bila malipo kufuatia kufanyiwa uhakiki kwa familia zisizojiweza.

Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Dr Faustine Ndugulile, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Taska Mbogo, ambaye alihoji juu ya wagonjwa hao kupewa matibabu ya bure.

Mbunge huyo  amehoji kuwa "Serikali ina mpango gani kuwasaidia wagonjwa wa Sickle cell (Seli mundu) ili watibiwe bure?"

Akijibu swali  Naibu Waziri wa Afya Dr. Faustine Ndugulile amesema kuwa "kupitia Wizara ya Afya tumeandaa muongozo wa kutoa msamaha kwa wagonjwa wa Sickle cell (Seli mundu), familia zisizojiweza zitahakikiwa na kupewa kibali cha huduma bila malipo. Serikali inaanzisha mpango wa taifa kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza."


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments