HII HAPA ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO, ELIMU YA KATI NA VYUO VYA UFUNDI KWA MWAKA WA MASOMO 2019
BOFYA HAPA KUONA MAJINA YOTE

Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano, Elimu ya Kati na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka wa Masomo 2019


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo amesema wasichana wote waliofaulu katika mtihani wa kidato cha Nne katika mwaka uliopita wa 2018 wamefanikiwa kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano pamoja na vyuo mbali mbali vya ufundi nchini.

Jafo, ametoa kauli hiyo hii leo mjini Dodoma wakati akitangaza wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano na vyuo vya elimu ya ufundi kwa mwaka wa masomo utakao anza mapema mwezi Julai, 2019.

“Nipende kuwatangazia habari njema kuwa, kwa mwaka huu wasichana wote waliofaulu wamefanikiwa kuchaguliwa kujiunga kidato cha tano pamoja na vyuo mbali mbali vya ufundi, ambapo jumla yao ni wasichana 45,816.

Akitoa takwimu za ufaulu wa watahiniwa wa kidato cha Nne kwa mwaka 2018, kuanzia daraja la kwanza hadi la tatu, alisema ni watahiniwa 113,825 kati yao wasichana ni 47, 779 na wavulana 66,046 sawa na asilimia 31.76 ya watahiniwa wote waliofanya mtihani.

Katika hatua nyingine Waziri Jafo, amezitaka Halmashauri hususan ni zenye tahasusi za masomo ya Sayansi na Hisabati kukamilisha madarasa ya kidato cha tano na sita ifikapo Machi, 2020, amezitaja Halmashauri hizo kuwa ni Kyerwa DC, Kilindi DC, Kilombero DC, Handeni DC, Malinyi, Mtwara DC, Momba DC, Nanyumbu DC na Nanyamba DC, huku akiwataka Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kusimamia kwa karibu na kuhakikisha azma ya Serikali kwa kila yakuwa na shule ya kidato cha tano inatimia.

Mwisho Waziri Jafo, amewataka Wanafunzi wote waliochaguliwa kuzingatia maelekezo yote muhimu ikiwepo kuthibisha kwao kabla ya tarehe ya mwisho hususan kwa wale watakao jiunga na vyuo vinavyo simamiwa na (NACTE).

“Tumetoa tarehe kuanzia 09 Juni, 2019 hadi 30 Agosti wote wawe wamethibithisha kujiunga katika vyuo vya ufundi na watakaoshindwa kufanya hivyo nafasi zao zitajazwa na wanafunzi wengine.” Alisema Waziri Jafo.

Ofisi ya Rais TAMISEMI, imekasimiwa jukumu lakusimamia zoezi la uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga kidato cha Tano pamoja na Vyuo vya ufundi kuanzia mwaka 2014 mara baada ya kutangazwa kwa Matokeo ya kidato cha Nne.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post