ALIYEKUWA KAMANDA WA POLISI AKUTWA AMEKUFA NJE YA NYUMBA YAKE

Aliyewahi kuwa kamanda wa polisi mkoa wa mjini magharibi Unguja, Azizi Juma Mohamed amekutwa amefariki dunia asubuhi ya kuamkia leo nje ya nyumba yake Kijichi Zanzibar.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumapili Juni 9, 2019, Kamishna wa Polisi, Zanzibar, Mohamed Hassan Haji amekiri kutokea kwa kifo hicho alichosema kina utata, kwa kuwa si cha kawaida.

Hata hivyo, amesema licha ya uwapo wa tetesi kuwa Azizi amejinyonga nje ya nyumba yake huko Kijichi, amesema hawezi kueleza kwa kina taarifa hizo kwa sasa.

Amesema bado ni mapema na wanaendelea na uchunguzi, baada ya kubainika sababu ya kifo chake watatoa taarifa zaidi.

“Naomba utosheke na hapo kwa sasa najua mnataka kujua kuhusu tukio hili na muda ukifika mtaelezwa kilichotokea,” amesema.

Mkuu wa kitengo cha uchunguzi kutoka Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja mjini Unguja, Dk Msafiri Marijani, amesema ni kweli wamepokea mwili wa ofisa huyo wa polisi hospitalini hapo.
Na Muhammed Khamis, Mwananchi 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post