RAIS WA SHIRIKISHO LA SOKA BARANI AFRIKA CAF AKAMATWA UFARANSA

Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) Ahmad Ahmad ametiwa mbaroni na mamlaka nchini Ufaransa ambako alikuwa akihudhuria Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

Taarifa ya kukamatwa kwake imethibitishwa na FIFA lakini haijaweka wazi sababu zaidi ya kusema “Tuhuma zake zinahusiana na mamlaka yake akiwa Rais wa CAF”.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa “FIFA haijui kwa undani uchunguzi unaofanywa dhidi yake kwahiyo haiwezi kusema chochote”.

FIFA imeziomba mamlaka zinazohusika na sakata hilo nchini Ufaransa kutoa taarifa kwenye kamati yake ya maadili.

Ahmad ambaye ni waziri wa zamani wa Madagascar aliripotiwa kwa kamati ya maadili ya fifa kwa madai ya ufisadi na unyanyasaji na katibu mkuu wa Caf Amr Fahmy. Baadaye Fahmy alifutwa kazi.

Ahmad mwenye umri wa miaka 59, alichukuliwa katika hoteli yake, mjini Paris mapema mwendo wa alfajiri na kuhojiwa na maafisa wa polisi wa Ufaransa wanaokabiliana na uhalifu wa kifedha na Ufisadi, kulingana na vyombo vya habari vya Ufaransa.

Ahmad ambaye pia ni naibu rais wa Fifa alikuwa nchini Ufaransa katika mkutano wa Fifa siku ya Jumatano ambapo rais wake mpya Gianni Infantino alisema kuwa shirikisho hilo limeondoa picha mbaya iliokuwa nayo..


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post