RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI WA WAKALA YA NISHATI YA UMEME VIJIJINI (REA)


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala ya Nishati ya Umeme Vijijini (REA), Michael Pius Nyagoga.

Taarifa ya Ikulu iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,  Ikulu Gerson Msigwa, utenguzi huo umeanza leo Juni 17, 2019.

Aidha kutokana na uamuzi huo, Rais Magufuli amemteua Wakili Julius B. Kalolo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala ya Nishati ya Umeme Vijijini (REA), kuanzia leo Juni 17, 2019.


 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527