RAIS MAGUFULI AMTUMBUA KAMISHNA WA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BIMA TANZANIA (TIRA)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Mussa C. Juma kuwa Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA).

Uteuzi wa Dkt. Mussa C. Juma umeanza June 25, 2019.

Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Mussa C. Juma alikuwa Mkuu wa Idara ya Bima katika Kitivo cha Bima na Hifadhi ya Jamii cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).

Dkt. Mussa C. Juma anachukua nafasi ya Dkt. Baghayo Abdallah Saqware ambaye uteuzi wake umetenguliwa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post