MWAKYEMBE AWAOMBA WATANZANIA KUICHANGIA STARS | MALUNDE 1 BLOG

Monday, June 17, 2019

MWAKYEMBE AWAOMBA WATANZANIA KUICHANGIA STARS

  kisesa       Monday, June 17, 2019


WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe, amewataka Watanzania kuchangia timu yao ya taifa ya soka, Taifa Stars inayojiandaa kushiriki Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON). 
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam, Waziri Mwakyembe amesema ni jukumu la kila Mtanzania kuchangia kiasi chochote kwa ajili ya kutoa hamasa kwa wachezaji.

Amesisitiza kwamba fedha zitakazochangwa si kwa ajili ya kuipeleka timu Misri na kuirudisha, “hatuhitaji kuwaweka kwenye hoteli nzuri (hayo yote yameshafanyika) tunahitaji kufanya kitu ili timu yetu ifanye vizuri.

Alisema kuwa kuna baadhi ya nchi zimetangaza kutoa magari na vitu mbalimbali nao wameamua kuanzisha kitu ambacho kitawapa morali vijana wao.

Alisema kuna akaunti mbili maalum ambazo zitakuwa zikiingizwa fedha hizo, ambazo ni CRDB no 01J109956700 na ya Baraza la Michezo Tanzania (BMT) 0111010009781 pamoja namba ya simu ya mkononi 0735414043 ya Oscar Zabron. 

Alisema siku ya Alhamisi watakuwa na hafla ya maalum ambayo itakuwa ya moja kwa moja, ikiwa ni pamoja na kuandaa vyeti maalum vya shukurani kwa watakaochangia.

 “Siku ya Alhamisi asubuhi tutakuwa na zoezi kubwa ambalo litaluwa LIVE kwenye mitandao na television mbalimbali na kwenye radio ambapo tutafanya uchangiaji wa Taifa Stars. 

Nawahakikishia kila shilingi itakayopatikana itakwenda kwa vijana wetu, wasishindwe kwa kuvunjika moyo,” amesema.
"Watanzania sio lazima uwe na uwezo kiasi chochote kile hata 2,500 inapokelewa na kuwepo sehemu ya zawadi kwa wachezaji wetu" alisema Mwakyembe.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post