MKOPO WA SHILINGI MILIONI 194 WATOLEWA KWA WANAWAKE, VIJANA NA WALEMAVU WILAYANI NJOMBE

Na Amiri kilagalila-Njombe

Jumla ya vikundi 86 vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu halmashauri ya wilaya ya Njombe vimepatiwa mikopo yenye thamani ya kiasi cha shillingi milioni 194 kwa mwaka wa fedha 2018/2019.

Mikopo hiyo iliyotolewa kwa awamu mbili,awamu ya kwanza halmashauri hiyo ilitoa mikopo ya thamani ya tsh milioni 66 mnamo mwezi february 2019 katika vikundi 36 huku awamu ya pili ikitolewa tsh milioni 128 katika vikundi 50.

Katika kipindi hicho cha 2018/2019 vikundi vya wanawake vimeonekana kuongoza kupatiwa mikopo kwa kuwa na vikundi 59,vijana 22,watu wenye ulemavu Vikundi 5

Akisoma taarifa ya mikopo ya awamu ya pili katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Ally Juma Ally, amesema kuwa kwa mwaka 2018/2019 halmashauri hiyo imeviwezesha vikundi 59 vya wanawake, vijana vikundi 22 na watu wenye ulemavu vikundi vitano.

Aidha mkurugenzi huyo amebainisha kuwa kati ya shilingi Milioni 194 zilizokopeshwa, milioni 143 ni mchango wa mapato ya ndani ya halmashauri, shilingi milioni 51 zinatokana na marejesho ya mikopo ya awali na kuongeza kuwa halmashauri hiyo imevuka lengo kwa kutoa mikopo kwa asilimia 135 kati ya asilimia 100 zilizowekewa malengo kwa mwaka 2018/2019.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Njombe Bi. Ruth Msafiri  ambaye alikuwa mgeni rasmi katika makabidhiano ya mikopo hiyo amewataka wanufaika wa mikopo hiyo kuitumia ipasavyo katika kujikwamua kiuchumi pamoja na kuirejesha kwa wakati ili Serikali kupitia halmashauri ya Njombe iendelee kutoa mikopo mingine kwa wahitaji.

Baadhi ya Wanufaika wa mikopo hiyo wakiwemo watu wenye ulemavu wameipongeza halmashauri ya wilaya ya Njombe kwa kutambua umuhimu wa vikundi vyao na kuvisaidi kupata Fedha ili waweze kuendesha shughuli zao za ujasiliamali kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527