MISRI YAANZA VIZURI MICHUANO YA AFCON KWA USHINDI WA BAO 1:0 DHIDI YA ZIMBABWE


Michuano ya 32 ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika imefungua pazia lake nchini Misri jana Ijumaa kwa mchezo kati ya wenyeji Mafarao wa Misri  dhidi ya timu ya taifa ya Zimbabwe.

Katika mchezo huo wa kundi A wenyeji Misri wameichapa Zimbabwe bao moja kwa bila mbele ya zaidi ya mashabiki 70,000 waliofurika katika uwanja wa kimataifa wa michezo mjini Cairo.

Kiungo wa timu ya taifa ya Misri, Mahmoud Trezeguet ndiye aliyewatoa kimasomaso wenyeji hao wa michuano ya 32 ya kombe la mataifa ya Africa wakati wa mechi hiyo ya ufunguzi iliyokuwa na shinikizo kubwa kutoka kwa mashabiki wa kandanda nchini Misri.

Bao lake la mnamo dakika ya 41 lilisadifu kuwa muhimu kuiwezesha timu yake kijinyakulia alama tatu za mapema katika fainali hizo zitakazoendelea karibu mwezi mzima.

Bao la Trezeguet liliibua shangwe na kuizima kwa muda nyota ya mshambuliaji mashuhuri anayeichezea ligi ya Premier Mohamed Salah ambaye alishangiliwa kwa nguvu mara zote alipougusa mpira.

Salah alipata nafasi mbili muhimu katika dakika za awali za mchezo na baadaye wakati wa kipindi cha pili lakini hakufanikiwa kutikisa nyavu za wazimbabwe.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post