MILIONI 370 ZAPATIKANA KATIKA HARAMBEE YA KUICHANGIA TAIFA STARS


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema kuwa mpaka sasa zimepatika Milioni 370 katika harambee ya kuichangia Timu ya Taifa Stars.


Makamu wa Rais amewapongeza Watanzania wote waliojitolea kuichangia Timu hiyo kiasi hicho cha Fedha ambapo harambee hiyo imefanyika leo  eneo la serena jijini Dar Es Salaam

Akizungumza mara baada ya Harambee hiyo kukamilika, Mama Samia alisema harambee imeonyesha mafanikio makubwa na anaamini litakuwa chachu kwa timu ya taifa kufanya vizuri kufanya vyema.


"Kazi tuliyoifanya hapa leo imetusogeza hadi Shilingi 370 milioni. Kampeni hii ni endelevu na itaendelea huko mikoani.

“Kampeni hii naamini inawajaza motisha kwa wachezaji wetu na kwa upande mwingine niwashukuru Watanzania wote kwa muitikio chanya na naomba waendelee kuchanga," alisema Mama Samia.

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) tayari kiko Misri kwaajili ya mashindano ya Africa, AFCON 2019 ambayo yanatarajiwa kutimua vumbi hapo kesho. 

Tayari Spika wa Bunge, Job Ndugai amewasili nchini humo kwaajili ya kuipa hamasa Timu hiyo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post