MFANYABIASHARA APORWA MIL 55 BAADA YA KUDAIWA KUNYWESHWA SUMU


Watu wawili wa familia moja, wanashikiliwa na Polisi Mkoani Mbeya kwa tuhuma za mauaji ya mfanyabiashara wa ufuta Oswald Malambo na kupora kiasi cha shilingi milioni 55.

Watuhumiwa hao ambao ni wakazi wa Kata ya Ifumbo Wilayani Chunya, inasemekana waliweka kitu kinachodhaniwa ni sumu kwenye kinywaji alichotumia mfanyabiashara huo, wakati wakiwa kwenye hotel baada ya kufanikiwa kuuza ufuta.

Kamada wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ulrich Matei, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi.

Kamanda, amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Raphael Walolile na Goliat Walolile.Amesema tukio hilo lilitokea Juni 2 mwaka huu na kwamba marehemu ndiye aliyetoa taarifa za kwamba alinyweshwa sumu na watuhumiwa lakini bado haijathibitishwa.

“Kwa sasa bado tunasubiri taarifa za daktari na kama itabainika ni sumu sheria zitachukuliwa dhidi yao ikiwa na kufunguliwa shitaka la mauaji,”

Aidha, akizungumzia hilo, Msemaji wa familia hiyo, Mhandisi Selemani Malambo, alisema ndugu yao alienda kuuza ufuta eneo la Mbalizi Halmashauri ya Mbeya, akiwa mzima lakini baada ya kuuza ufuta wakati akijiandaa kurudi aliombwa na watuhumiwa wakafanye mazungumzo.

Mhandisi Malambo amesema watuhumiwa walimtaka ndugu yao huyo wakazungumze naye kwenye moja ya bar zilizopo katika eneo la Kabwe Jijini Mbeya na alipofika katika eneo hilo, watuhumiwa hao, walimtaka awaache wadogo zake nje jambo lililofanyika.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post