MAREKANI YASHAMBULIA MIFUMO YA KOMPYUTA YA SILAHA ZA MAKOMBORA ZA IRAN


Marekani imefanya mashambulizi ya mtandao kwenye mifumo ya silaha za Iran na kuiharibu kabisa.

Tukio hilo limefanywa siku chache baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump kutangaza kuachana na mashambulizi ya anga katika nchi hiyo yenye lengo la kulipiza kisasi.

Jumanne iliyopita Iran iliitungua ndege ya Marekani isiyokuwa na rubani kwa madai kuwa ilipita katika anga lake jambo ambalo lilipingwa na Rais Trump na kudai kuwa ilikuwa katika anga la kimataifa.

Gazeti la Washinton Post limeripoti leo June 23, kwamba nchi hiyo imeharibu mifumo ya kompyuta inayodhibiti roketi na mitambo ya kurushia makombora ya Iran.

Kwa mujibu wa gazeti la New York Times, tukio hilo ni kulipiza kisasi kufuatia mashambulizi mawili yaliyofanywa na Iran ikiwamo lile la kuteketezwa kwa meli ya mafuta kwenye Ghuba ya Oman.


Trump ameahidi kuiwekea Iran vikwazo vipya zaidi kuanzia kesho Jumatatu.


 Lakini Iran nayo imeionya Marekani kuwa shambulizi lolote dhidi yake litawafanya washirika wa Marekani walioko Mashariki ya Kati kuona moto.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527