Mwendesha bodaboda aliyejulikana kwa jina la Vincent Okoth mkazi wa eneo la Rachuonyo kaunti ya Homa Bay nchini Kenya amenusurika kufa baada ya kikundi cha vijana kutaka kumuua kwa kumpiga mawe.
Imeripotiwa kuwa mshukiwa alimbaka mteja wake wa kike aliyetaka ampeleke kwa mpenziwe usiku wa Jumanne Juni 12,2019.
Wahudumu wenzake wa bodaboda wanasemekana kughadhabishwa na kitendo hicho cha Vincent Okoth ambapo pia walitaka kumuadhibu kwa kuwachafulia sifa.
Joshua Owiti alisema Okoth alimbaka mwanamke huyo aliyekuwa amesafiri kutoka Narok kwenye chumba kimoja katika kijiji cha Jwelu.
Mwathiriwa alipelekwa katika hospitali ya Homa Bay ambapo ilithibitika kuwa alibakwa baada ya kufanyiwa vipimo.
Kulingana na taarifa za edaily, mshukiwa alikamatwa na anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Othoro huku uchunguzi zaidi ukianzishwa dhidi yake.
Chanzo Tuko