MAPACHA WAOLEWA NA MAPACHA WENZAO


Ilikiwa tarehe 25 Mei ,2019, mamia ya watu walipokusanyika katika kijiji cha Rugando nchini Uganda katika sherehe ya kutoa mahali ya wasichana mapacha , Bi Priscilla Babirye na Bi Pereth Nakato mabinti wa marehemu Late Kaddu Ssalongo kutoka kijiji hicho.

Walikuwa wanatolewa kwa Bwana Asiimwe Edward mfanyabiashara katika mji wa Mbarara mashariki mwa Uganda na Bwana Amos Besigye Kutoka wilaya ya Ntungamo ambaye ni mvuvi katika wilaya ya Rwampara .Maharusi
La kushangaza ni kwamba, mabwanaharusi, pia walikuwa ni mapacha , ingawa walikuwa wakitoka katika familia tofauti.
Safari yao ya mapenzi

Nilikuwa nimeenda kwenye mazishi ya mke wake na rafiki yangu ambaye alisomea mafunzo ya uuguzi na Nyakato.

Nilikuwa nimeenda kule kumfariji bwana na Nakato na dada yake walikuwa wameenda kumfariji mke wake. Nilikuwa nimeketi kwenye hema kama mgeni rasmi na mbele yangu nikamuona msichana mrembo akiwa amesimama.. alikuwa anapigwa na jua.

Nilimuita mshichana huyu na nikamuomba aje tuketi pamoja kwneye kiti changu. Baada ya kukaa, nilishangaa kumuona mtu kama yeye sura kama yake akiwa amesimama mahali pale pame alipokuwa amesimama .

Mtu mmoja akaniambi aah! ni mapacha. Ilibidi nivute kiti kingine ili nikae nao wote wawili. Wakati huo sikusema lolote.Nyakato na Besigye

Baadae nilimuomba rafiki anipatie namba zao za simu. Na kile ambacho ningekifanya nikuwatumia tu ujumbe.

Baadae nikabaini kuwa alikuwa anafanya kazi katika duka la dawa karibu na nyumbani kwetu , ikanibidi niwe na mazowea ya kwenda nyumbani kila wikendi ili niweze angalau kumuona.

Nyakato: Tulikutana kwenye mazishi katika kijiji cha Ibanda. Baadae nikapokea jumbe zake za simu na siku zijibu lakini hakukata tamaa . Mimi na dada yangu tulikuwa tumekubaliana tangu zamani tukiwa shule ya msingi kuwa tutaolewa siku. Aliponiambia kuwa anachumbiwa na mwanamme, ilinibidi niwe makini pia.

Alikuwa ananiletea ice cream kwenye boksi lenye picha za dawa za wanyama, biskuti na zawadi nyingine ndogo.

Babirye: Nilikuwa nimesoma shule moja na yeye ya Trinity College iliyopo wilayani Kabale ambako nilizomea na pacha yangu -dada yangu. Hatukuwa na hatukuwahi kuzungumza. Tulikuwa tunatoka kwenye mazishi katika kijiji cha Ibanda tarehe 16 Disemba, 2017 na dada yangu na tulipokuwa tunatoka kwenye mazishi tukakutana na Edward. Akaomba siku yangu ambayo nilimpatiaBabirye na Edward

Baadae akaanza kunipigia simu na kuninong'oneza maneno mataamu maskioni mwangu.

Nilimshirikisha dada yangu jumbe alizokuwa akinitumia, ambaye pia aliniambia kuwa mwanaume ambaye tulikuwa tumekutana kwenye matanga alikuwa. Sote tukaamua kuwa makini na mahusiano yetu.

Edward: Nilipokutana na mapacha , nilianza kumpigia simu Babirye lakini aliskika kama mtu ambaye hakuwa na utashi. Nilitaka kumuoa pacha kwasababu mimi pia ni pacha kwa hiyo sikukata tamaa niliendelea kujaribu bahati yangu.

Besigye: Tuliendelea kujaribu bahati yetu lakini hatukujua kuwa wasichana walikuwa wanatumiana jumbe za yale tuliyokuwa tunawaambia . Wakati mambo yalipofika mbali , walituomba tukutane na kubadilishana mawazo juu ya namna tutakavyopata pesa na jinsi tutakavyozitumia na mambo mengine.Bwana Edward Asiimwe wa 2-(kushoto) na Bwana Amos Besigye wa 2 (kulia) wakiwa pamoja na wakiwa pamoja na wasindikizaji wao wakati wa sherehe ya kutoa mahali

Edward: Tuliendelea kuwasiliana hadi akaja kunitembelea. Aliponitembelea kwa mara ya kwanza, nilikuwa na uhakika kuwa lazima atakuwa wangu na aliponitembelea mara ya pili tulikuwa tunajadili juu ya namna tutakavyokuwa na sherehe.

Babirye and Nakato: Kwasababu tulikutana nao siku moja , tuliendelea kuzungumzia kile kuhusu matanga na kupoteza muda ili tuone kama ndoto yetu ya kuwa na sherehe ya harusi siku moja itatimia.Mama yake na Bwana Besigye akiwa pamoja na pacha wake wakati wa sherehe za kutoa mahali

Mwaliko wa sherehe ya kutoa mahali.

Besigye na Edward: Tuliombwa sote tulete wageni 40 kila mmoja.

Babirye na Nakato; Tulipanga kuwaalika watu 600 lakini idadi ilizidi hiyo. Kwa kiasi kikubwa jukumu la kuwaalika watu waliachiwa wazee ambao walitaka kuendeleza jina la marehemu baba yetu. Hii ilikuwa rahisi zaidi, lakini tulikuwa na malalamiko mengi kutoka kwa marafiki zetu ambao hawakualikwa. Tunatumai watahudhuria harusi .

Kuhusu keki je?Babirye na Nakato waliamua kutengeneza keki moja ili kaka yao awasaidie kuikata

Babirye na Nyakato: Tulikuwa na keki moja kwasababu tulikuwa na kaka mmoja ambaye tungekata nae keki.
Mabwana harusi walileta zawadi tofauti kwa familia?Mapacha wakitoa zawadi kwa mjomba waoKila Bwanaharusi alilileta kilo 50 za sukari na zawadi nyingine kwa ajili ya familia za wachumba wao

Besigye na Edward: Tulikutana kabla ya sherehe rasmi na tukakubaliana juu ya zawadi tutakazowapa wazazi wa wachumba , lakini kila upande ulibeba zawadi zake. Kama ilikuwa ni kteti nne za bia, mmoja alileta kreti mbili na mwenzake vivyo hivyo. Kila mmoja wetu alileta kilo 50 za sukari,. Na tulifanya hivyo hivyo upande wa soda na zawadi nyingine. Lakini huu ulikuwa ni mpango wetu wenyewe kama mabwanaharusi . Lakini kila familia ilikuja imebeba zawadi zake tofauti.

Walichagua vipi rangi ya siku yao?.Askofu wa Ankole George Tibesigwa waliwabariki mapacha

Nyakato: kwasababu Babirye ni mkubwa kwangu walau kwa kuzaliwa dakika chache kabla yangu, ilibidi nimruhusu aongoze katika baadhi ya maamuzi. kwa bahati nzuri sote tlipendelea mambo sawa tulipenda rangi zinazofanana . Tulichagua mapambo ya rangi ya dhahabu na nyekundu(damu ya mzee). Hizi ni rangi ambazo tulizipenda tangu utotoni.Kikundi cha Afrii Doves kiliwatumbuiza wageni
Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527