MWENYE NYUMBA APEWA KICHAPO NA MPANGAJI KISA KUDAI KODI YA NYUMBA USIKU

 Uhusiano kati ya wenye nyumba na wapangaji wao wakati mwingi huwa sio mzuri, hasa wakati kodi ya nyumba inapochelewa, wenye nyumba na maajenti wao hutumia mbinu zote zikiwemo zisizofaa kudai pesa zao. 

Hata na wengine huja usiku ama kuwafungia milango kwa kufuli wapangaji wao katika kudai kodi.

 Katika Kaunti ya Nakuru,nchini Kenya George Shiundu, ambaye ni mwenye nyumba, alikuwa amechoshwa na mchezo wa paka na panya ambao mpangaji wake kwa jina Yohana Sunday alikuwa akiucheza na hapo akaamua kumtembelea usiku.

 Safari yake iligeuka kuwa tukio baya baada ya Sunday kumshambulia huku akiwalazimisha majirani kuingilia kati kumnusuru mwenye nyumba. 

Inaelezwa kuwa, George Shiundu mwenye nyumba, alishambuliwa na Yohana Sunday, mpangaji wake Mei 20 
 baada ya kufika mlangoni pa Sunday kudai kodi.

 Sunday ambaye alikuwa amepangisha nyumba katika mtaa wa Kaptembwo kaunti ya Nakuru aliingia mitini baada ya kupata fununu kuwa mwenye nyumba alikuwa amefika polisi kumshtaki kufuatia tukio hilo. 

Kulingana na taarifa katika gazeti la Daily Nation, polisi walianzisha msako kumtafuta Sunday na hatimaye wakamtia mbaroni.

Alipofikishwa kortini mjini Nakuru, ilibainika kuwa Sunday alimvamia kwa ngumi na mateke mwenye nyumba aliyekuwa amefika kudai kodi ya nyumba Mei 20, 2019.

 Upande wa mashtaka umesema kuwa mshukiwa alikerwa na kitendo cha kubishiwa mlango usiku na mwenye nyumba aliyekuwa akidai kodi ambayo ni kweli ilikuwa imechelewa kulipwa. 

Jumatatu, Juni 10, Hakimu Bernard Mararo hatimaye alimpata mshukiwa na kosa la kumudhuru Shiundu na kumuumiza. Sunday alikubali mashtaka dhidi yake na hakimu kuamrisha kesi hiyo kutajwa tena mwezi Juni 24,2019.

Chanzo Tuko

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527