AOMBA MSAADA SERIKALINI BAADA YA KUNYOFOLEWA NYETI ZAKE NA FISI

Jamaa aitwaye Julius Somoire (26) aliyenusurika kifo baada ya kuvamiwa na kuumwa na fisi sehemu zake za siri kaunti ya Kajiado nchini Kenya ameitaka serikali kumfidia kufautia majeraha mabaya aliyoyapata.
 
Mbali na kumjeruhi sehemu zake za siri, fisi huyo pia alimuuma kwenye mikono na miguuni alipojaribu kuwaokoa mifugo wake aliokuwa akiwachunga eneo la Isinya Jumamosi, Juni 22,2019. 

 "Fisi huyo aliniuma sehemu zangu za siri, aliniumiza sana na sijui iwapo nitarejelea hali yangu ya kawaida, pia aliniuma kwenye miguu na mikono na kuniacha na majeraha mabaya, " Somoire alisema. 

Somoire alikimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Kajiado huku wakazi wa Isinya wakifanikiwa kumuua fisi huyo kwa kumpiga kwa rungu na mawe.

 Shirika la Wanyama Pori, KWS kwa shambulizi hilo na kulitaka litafute suluhu ya haraka ya kuwazuia wanyama pori kuwavamia wakazi.

 Aidha, wakazi hao sasa wanataka Somoire afidiwe wakidai shirika hilo limetepetea kazini na linaweka hatarini maisha ya binadamu.
Chanzo- Tuko

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post